Nyumba
inayomilikiwa na serikali ya Zimbabwe imeuzwa $280,000 (£180,000) kupitia mnada
Afrika Kusini.
Mwekezaji katika nyumba Arthur
simatakopoulos amenunua nyumba hiyo iliyoko mji wa Cape Town, kwa mujibu wa
mwandishi wa BBC Mohammed Allie.
Mnada huyo umefanyika baada ya
serikali hiyo kushindwa kwenye vuta nikuvute iliyodumu miaka mitano na shirika
la kutetea haki za Waafrikaner nchini Afrika Kusini kwa jina AfriForum.
Shirika hilo liliitaka serikali
ya Zimbabwe kulipa gharama ya kesi baada ya serikali hiyo kushindwa kwenye kesi
iliyohusu mageuzi ya umiliki wa mashamba.
Serikali ya Zimbabwe chini ya
Rais Robert Mugabe ilikuwa imechukua mashamba kutoka kwa Wazungu na kuyapa
Waafrika weusi.
Mahakama maalum ya muungano wa
mataifa ya Afrika Kusini (Sadc) iliamua 2008 kwamba mpango huo ulikuwa kinyume
cha sheria, shirika hilo lilisema.
Mahakama Kuu mjini Pretoria
iliwaagiza maafisa nchini Afrika Kusini kutwaa mali hiyo 2010.
Zimbabwe ilifika kortini mara
kadha kupinga uamuzi huo bila mafanikio.
0 comments:
Post a Comment