Friday 4 September 2015

Mamilionea wengi wanapatikana Africa kusini.....

Mji wa JonannesburgMji wa Johannesburg nchini Afrika Kusini, ndio mji ulio na idadi kubwa zaidi ya watu tajiri barani Afrika.
Haya ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na benki ya Afr Asia na jarida la New World Wealth.
Mji huo unaofahamika kwa mji wa dhahabu,ina watu wapatao elfu 23 na mia 4 ambao ni mamilionea.
Inakisiwa kuwa asilimia 30 ya mamilionea barani Afrika wanaishi Afrika Kusini.
Misri ni ya pili ikiwa na mamilionea elfu 10 na mia 2, Nigeria ni ya tatu ikiwa na mamilionea elfu 9 na mia 1.
Utafiti huo umechukua takwamu ya watu ambao wana zaidi ya dola milioni moja pekee.
Ripoti hiyo inakadiria kuwa barani afrika kuna mamilionea laki 1 na elfu 63,ambao kwa pamoja mali yao yote inakisiwa kuna dola bilioni 670.
Inashangaza kuwa mji wa Johannesburg una idadi kubwa na mamilionea kuliko Lagos, mji ambao unakisiwa kuwa mji mkubwa wa biashara barani Afrika,kwa sababu Nigeria pia ina idadi kubwa zaidi ya watu na uchumi wake ndio mkubwa zaidi barani Africa.

Lakini licha ya utajiri huu wote Afrika Kusini,bado ingali inakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira na umasikini.

0 comments:

Post a Comment