Watu
wengi Ulaya ni wanene kupita kiasi, kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya
Duniani (WHO).
Ripoti hiyo kwa jina European
Health Report inasema 59% ya watu wanaoishi ulaya, wana uzani uliozidi au ni
wanene sana.
Shirika hilo limesema eneo la
Ulaya lililochunguzwa, ambalo hujumuisha baadhi ya maeneo ya bara Asia, ndilo
lililokuwa na viwango vya juu zaidi vya unywaji pombe na uvutaji sigara
duniani.
Kutokana na hayo maafisa wa WHO
wameonya kuwa huenda vijana wa eneo hilo wasiishi muda mrefu kama walivyoishi
mababu zao.
Hata hivyo imeonya kuwa 30% ya
watu eneo hilo,bado wanavuta sigara, kiwango ambacho kinazidi maeneo mengine
yote.
Mkurugenzi wa WHO anayesimamia
Ulaya suzanna Jakab amesema,Ripoti hii imeonyesha matumaini. Lakini bado kuna hatari
iwapo uvutaji sigara na unywaji pombe utaendelea kwa viwango vya sasa.
0 comments:
Post a Comment