Wanasayansi wametangaza kuwa kuna ushahidi wa kuaminika kuwa,kuna maji katika sayari ya Mars na hivyo kuibua matumaini kuwa kuna uwezekano wa viumbe kuishi katika sayari hiyo.
Wataalamu kutoka taasisi ya utafiti wa safari za anga
ya juu ya Marekani NASA, wamesifu ugunduzi huo wa wanasayansi na kusema kuwa, unatoa
ufahamu zaidi kuhusu sayari ya karibu na dunia kuwa sio kavu kama ilivyodhaniwa
hapo awali.
Mkurugenzi wa NASA Jim Green, amewaambia wanahabari
mjini Washington Marekani kuwa, kugundulika kwa maji katika sayari ya Mars ni
habari njema kuwa viumbe hai vinaweza kuishi katika sayari hiyo.
0 comments:
Post a Comment