Papa
Francis anatarajia kurahisisha taratibu zinazoruhusu wafuasi wa kanisa katoliki
waliooana kutoa talaka na kuolewa tena huku wakibakia kuwa wafuasi wa katika
kanisa hilo.
Maelezo ya taratibu hizo
yanatarajiwa kutangazwa mjini Vatcan baadaye leo.
Papa aliunda tume ya wanasheria
wa kanisa mwaka jana, kupiga msasa mbinu ya kurekebisha taratibu hizo
zinazoruhusu wanandoa kuachana na kupunguza gharama.
Bila sheria hiyo wanandoa wa kikatoliki wanaotalikiana na
kuolewa upya, hutazamwa kama wazinifu na hawaruhusiwi kupokea komunio.
Mwandishi wa BBC mjini Vatican
anasema kuwa Papa Francis hatabadilisha mafunzo ya katoliki kuhusu kuachana kwa
wanandoa,lakini atawezesha kurahisisha wanandoa wenye matatizo kuthibitisha
kuwa ndoa yao haikuwa ya maana tangu mwanzo
0 comments:
Post a Comment