Mahakama
ya Singapore imemuhukumu muuguzi mmoja kutoka nchini Ufilipino kifungo cha
miezi minne kwa kuchapisha maoni ya uchochezi kuhusu taifa hilo.
Ello Ed Mundsel Bello ambaye
amekuwa akifanya kazi nchini Singapore aliandika kwamba raia wa taifa hilo
hawako huru.
Alishtakiwa kwa kuwa muhaini na
kuwadanganya maafisa wa polisi.
Akitoa hukumu hiyo jaji huyo
alisema kuwa mahakama hiyo haikuweza kupuuza tishio la maoni hayo kwa jamii
ilio tulivu.
Singapore ni taifa lenye raia wa
mataifa na rangi mbali mbali na mamlaka hujali sana maoni ambayo yanaweza
kuchochea wasiwasi wa kibaguzi.
0 comments:
Post a Comment