Mandela alihamishiwa gereza la Pollsmoor kutoka Robben Island 1982 |
Watu karibu elfu 4
wameondolewa kutoka jela ya Pollsmoor nchini Afrika Kusini,baada ya panya wengi kuvamia gereza hilo na kusababisha kifo cha mfungwa
mmoja.
Kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Nelson Mandela aliwahi
kufungwa katika gereza hilo.
"Tumekuwa tukipuliza dawa,
lakini kwa sasa, tumelazimika kuwahamisha wafungwa, na itatuchukua siku kadha,”
msemaji wa jela hiyo Manelisi Wolela amesema.
Panya hao wameeneza maradhi
yajulikanayo kama leptospirosis, yanayosambazwa kupitia mkojo wa wanyama hao
waharibifu.
Muungano wa kutetea haki za
maafisa wa polisi na maafisa wa magereza umesema gereza hilo lilikuwa limejaa
kupindukia na hali ni ya “kinyama”.
Bw Mandela alihamishwa kutoka
jela ya Robben Island na kupelekwa Pollsmoor mwaka 1982
Maafisa wa afya wanasema hakuna
mtu afaaye kurejeshwa kwenye gereza hilo,hadi panya wote waangamizwe.
0 comments:
Post a Comment