This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Tuesday, 9 June 2015

Mguu bandia wenye hisia wazinduliwa......!!!



 
Watafiti katika chuo kikuu nchini Ausralia,wamevumbua mguu wa kwanza bandia duniani wenye uwezo wa kusisimua hisia halisi za binadamu.

Watoto kunufaika na dawa mpya za ARV…


Dawa za sasa zinaelezwa kuwa na ladha nzuri kuliko zinazotumiwa hivi sasa

 Watoto walioathirika na Virusi vya Ukimwi watanufaika kutokana na uamuzi wa mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani kuidhinisha dawa mpya ambazo zinaweza kuchanganywa kwenye Chakula

Bahari ni kubwa lakini ustahimili wake wa uchafuzi ni mdogo…



 
Licha ya kwamba eneo la bahari duniani ni kubwa,bado uwezo wake wa kustahimili uchafuzi utokanao na shughuli za binadamu ni mdogo.

Sikiliza Antenna show ya Tar 5-6-2015 hapa with Kiwa Strong..

KIWA STRONG "KIWALE 11"
Show inakujia kila siku za juma tatu mpaka ijumaa kuanzia saa kumi jioni mpaka saa kumi na mbili na nusu jioni,ndani ikiwa na mchanganyiko wa habari,matukio,mahojiano na burudani mbali mbali.
Hapa chini nimekuwekea shoy ya Tar 5-6-2015 unaweza kuisikiliza kwa kubonyeza play au kuidownload.
 

Mtandao wa kijeshi Marekani wadukuliwa...!!!!


Mkuu wa viongozi wa kijeshi nchini Marekani akiwa na waziri wake wa ulinzi Ash Carter

Jeshi la Marekani lilisimamisha kwa muda mtandao wake baada ya kisa cha kuingiliwa kimitandao.

Monday, 8 June 2015

UN:Eritrea imekiuka haki za binadamu............!!!!


 Umoja wa Mataifa unasema kuwa serikali ya Eritrea inaendesha ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya watu wa nchi hiyo.

Nyuki abadili safari ya ndege...!!!


Abiria wa ndege moja ya shirika la ndege la Flybe linalohudumu nchini Uingereza, walicheleweshwa kwa zaidi ya saa mbili baada ya wahandisi wa ndege hiyo kubaini kuwa nyuki alikuwa amepenyeza na kuingia ndani ya mitambo ya ndege hiyo na hivyo safari haingewezekana.

Friday, 5 June 2015

Marekani kuidhinisha 'Female Viagra'..!!!!


Viagra ya wanawake kuidhinishwa nchini Marekani

Jopo la serikali ya Marekani limewaagiza wasanifu kuidhinisha dawa ya kutibu hamu ya chini ya kiwango cha ngono, miongoni mwa wanawake inayojulikana kama ''Female Viagra''.

Data za wafanyakazi milioni 4 zadukuliwa Marekani….!!!



Serikali ya Marekani imethibitisha habari ya kudukuliwa taarifa za karibu wafanyakazi milioni nne wa serikali ya nchi hiyo.

Ghana yatangaza siku tatu za maombolezo...!!!!!

Kituo cha mafuta kikiwa kimeteketea mjini Accra, Ghana
Ghana imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo vya watu mia na hamsini vilivyotokana na mafuriko na mlipuko kwenye kituo kimoja cha mafuta.
Mlipuko huo ulitokea hapo jana wakati mamia ya watu walipokuwa wamejihifadhi katika kituo hicho cha mafuta kutokana na mvua kubwa zinazonyesha.
Rais wa Ghana,John Mahama amesema janga halitajirudia tena.
Moto ukiwaka kutokana na mlipuko uliotokea kituo cha mafuta na gesi mjini Accra, Ghana
Bwana Mahama amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mji mkuu ,Accra alipotembelea eneo la tukio.
Amesema watu wanapaswa kuachana na tabia ya kujenga kwenye mikondo ya maji na inabidi utekelezaji ufanyike ili kuzuia janga lingine kama hilo kutokea.
"Tutachukua hatua fulani kuzuia hili lisitokee katika wakati ujao na mara kwa mara. Hatua hizi zinapokuwa kali, mnakuwa na huruma na kutaka zisitekelezwe.
Lakini nafikiri wakati umefika, mnafahamu, kwa kuziondoa nyumba katika maeneo ya maji na umma lazima uelewe kuwa ni lazima kila mtu kuhudumiwa.
Nina maana kupotea kwa maisha kwa namna hii ni janga kubwa ambalo halijawahi kutokea hapo kabla."Anasema Rais Mahama.
Miili ya watu imeendelea kutolewa kutoka eneo la tukio na kuwekwa katika malori. Serikali ya Ghana bado inajaribu kupata idadi kamili ya watu waliokufa au kuathirika kutokana na ajali hiyo.
Wengi wa waliokufa walijihifadhi katika kituo cha petroli kukwepa mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha ambayo imesababisha mafuriko katika sehemu kubwa ya mji wa Accra.

Wanawake na wanaume walumbana Saudia.....!!!!

 
Wasaudi wamekuwa wakilumbana kwenye mtandao baada ya wengi wao kujitokeza kuchangia ujumbe uliowekwa wiki hii wenye maneno na na nukuu " Don't marry a Saudi man", yaani ole wako uolewe na Msaudi.

Thursday, 4 June 2015

Shule 700 zafungwa Korea Kusini……!!!



Rais wa Korea Kusini Park Geun-Hye

Zaidi ya shule 700 Korea Kusini zimefungwa kuhofia kuenea kwa ugonjwa uliozuka, unaoshambulia mfumo wa upumuaji uliozuka kutoka Mashariki ya kati wa MERS.

Mwigizaji wa filamu ya Godzilla afariki…!!!



 
Hiroshi Koizumi msanii wa Japan ambaye aliigiza katika filamu nyingi za Godzilla,amefariki akiwa na umri wa miaka 88.

Moto waua watu 96 Accra Ghana…!!!



 
Mlipuko wa moto katika kituo cha mafuta, Accra Ghana umeua watu 96 na uchunguzi zaidi unaendelea.

Marekani yakiri kutuma kimeta zaidi…..!!



 
Maofisa wa ulinzi nchini marekani wamekiri kuwa maabara kadhaa zilizopokea kimakosa sampuli hai za vidudu hatari vya kimeta ni zaidi ya mara mbili ya matarajio ya awali.