This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Tuesday, 25 September 2012

Watanzania mabingwa wa kiswahili?

Kwa mpenzi yeyote wa Kiswahili ni sharti azingatie stadi nne za lugha hiyo. Yaani kuzungumza, kusoma kuandika na kuelewa lugha ya Kiswahili. Hata hivyo baadhi ya wakenya wamekuwa wakilamika kuwa vitabu vingi vya Watanazani vimekuwa vikitahiniwa nchini Kenya hususan katika vidato vya tatu na vinne. Ukweli ni kuwa Watanzania wamewabwaga wakenya na ipo mifano ya kutajika kuhusiana na hilo katika vitabu hususan vya fasihi. Swali ni je Wakenya wamepewa fursa ya kuandika au la? Ni nani anastahili kuwaambia waandike vitabu vya Kiswahili, na je wachapishaji vitabu wako radhi kuzichapisha kazi za Wakenya? Kuanzia miaka ya themanini hadi sasa, idadi ya vitabu vya Watanzania vilivyotahiniwa katika kunga za riwaya, tamthilia na ushairi ni kubwa kushinda vya Wakenya. Riwaya ya Kusadikika ya Shaaban Robbert(Mtanzania) ilitahiniwa mwanzoni mwa miaka ya tisini hadi mwaka 1994. Wakati huo hadi mwaka 1997 tamthilia ya Mashetani ya Ebarahim N. Hussein(Mtanzania) ilitahiniwa. Mwaka wa 1994 hadi mwaka 1998 riwaya ya Kisima cha Giningi ya Mohamed Said Abdullah(Mtanzania) ilitahiniwa. Katika miaka hiyo kuanzia mwaka 1998 tamthilia ya Amezidi ya Said Ahmed Mohamed (Mpemba) ikaanza kutahiniwa kuchukua mahali ya tamthilia ya Buriani ya A. S Yahya na David Mulwa(Wakenya). Wakati huo Mkenya Khaemba Ongeti alijipenyeza na tamthilia yake ya Visiki. Hayakuishia hapo, baada ya tamthilia za Visiki na Amezidi kuondolewa katika ratiba ya shule za upili nchii Kenya ikaingia riwaya nyigine ya Mohamed Said Ahmed (Mpemba) ya Kitumbua kimeingia mchanga. Na hiyo ilipoondoka ikaja riwaya ya Utengano ambayo inatahiniwa hadi sasa. Ukweli unaojitokeza hapa ni kuwa taasisi ya elimu nchini haiviteui vitabu hivyo kwa sababu ni vya Watanzania. Ni kutokana namna vilivyosukwa kimaudhui na kifani.Isitoshe waandishi wa vitabu hivyo wameandika wameandika vitabu vingi tu. Kwa mfano Said Ahmed Mohemed ameandika zaidi ya vitabu 40 vya Kiswahili. Mohamed Said Abdullah ameandika vitabu vingi tu kama vile Kisima cha Giningi, Duniani kuna watu, Mizimu ya watu wa kale na Kadhalika. Hata hivyo ni vyema kutambua kuwa baadhi ya Wakenya wamejitokeza na kuandika kazi nzuri za fasihi ya Kiswahili kama vile Siku Njema ya Ken Walibora, Mstahiki Meya ya Timothy Arege na Kifo Kisimani ya Kithaka Wamberia. Kwa ufupi wapenzi wa Kiswahili katika kanda ya Afrika Mashariki wakijumuisha mataifa ya Rwanda, Sudan Kusini, Sudan, Somalia na Uganda waandike vitabu zaidi vya Kiswahili. Twasubiri siku watanzania watavitahini vitabu vya Kiswahili vya wakenya, Vivyo hivyo si dhambi kitabu cha Kiswahili kilichoandikwa na Mrundi ama Mnyarwanda kikitahiniwa Uganda na vinginevyo. Ni maoni tu!!!!

USOMAJI WA VITABU WAPUNGUA KWA SABABU YA MITANDAO YA KIJAMII???

Nimejikuta natafakari jambo hili na kuingia kwenye marumbano makubwa na serikali ya kichwa changu hasa nikiangalia hali halisi tunayoishi sasa. Mapinduzi ya kompyuta yamebadilisha sana maisha. Enzi zile hata ukipewa assignment darasani unakimbia maktaba kutafuta kitabu. Siku hizi mambo yamebadilika. Hata assignment inapotolewa wanafunzi wanakimbilia kwenye Internet maana vitu vinapatikana kwa urahisi zaidi. Najiuliza kwa staili hii kweli watu hasa walio na access ya Internet wastani wao wa kusoma vitabu ukoje? Ripoti moja ilishawahi kuonyesha kuwa ujio wa smartphone na mitandao ya kijamii inawashawishi sana watoto wasome vitabu. Ilinipa wakati mgumu sana kuitafakari ripoti hii iliyotolewa kutokana na utafiti mmoja nchini Marekani. Nikiangalia mazingira yetu inanipa wakati mgumu sana kuamini jambo hilo. Naona kama vile uwezo na hamu ya watu kusoma vitabu unapungua zaidi wakipendelea kuingia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kusoma hiki na kile! Hii ndiyo Teknolojia Yetu…

Sunday, 23 September 2012

HUTOKA KIWALENIIii HIKI HAPA KICHWA KINGINE...(KIWA WA 2)ANAWAKILISHA DH CREW-MWITE HUBE KIWA...

SIKILIZA NGOMA YAO HAPAA INAITWA SIKUDHANI...
HUBE KIWA(sapremo wa kili)ANAWAKILISHA DH.CREW(ODEO & HUBE)

Tuesday, 18 September 2012

TAHADHARI KWA WATUMIAJI SIMU ZA MKONONI

Simu zinatumia Mionzi ya MICROWAVE ambayo huwezesha kuunganisha simu yako kwenda kwenye Mnara na mnara huunganisha Simu yako na Mitambo ya Mtandao wako ambapo pia Hurudishwa kwenye mnara hadi kwa mtu Unaye mpigia. Microwave ndio njia kuu ya muunganisho huo Lakini kunamdhara mengi mtu huyapata kutokana na kuwa karibu na Mionzi hiyo ambayo hadi sasa bado haijafahamika ni kwa kiasi Gani. Uchunguzi umeonyesha kuwa kuna madhara mengi ya kiafya tunayapata kutokana na Matumizi ya simu. mfano wa magonjwa hayo ni 1.KUUMWA KICHWA MARA KWA MARA 2PRESSURE YA KUPANDA NA KUSHUKA 3.UVIMBE KWENYE UBONGO 4.KANSA 5.ALZHEIMER 6.NA MENGINE MENGI Hatuwezi kujizuia kutumia simu na Hatuwezi kuzuia hiyo mionzi ya MICROWAVE sababu ni sehemu ya shughuri zetu za kila siku ila tunaweza KUPUNGUZA. hapa nawaletea Njia chache za kupunguza Mionzi ya MICROWAVE isituletee matatizo makubwa zaidi. 1.Punguza matumizi yasio lazima ya simu. Mfano Ongea mda mfupi kwa kutumia simu sio muda mrefu uweunaongea,Uchunguzi umeonyesha kuwa ukiongea kwa DAKIKA mbili haileti madhara, (Alter natural electricity of the Brain) 2.Watoto wasiruhusiwe kutumia Simu bali pale tu inapobidi. 3.Tumia Earphone za wireless mfano za bluetooth. ni nzuri zaid kuliko za wire,Earphones za wire zinaongeza wingi wa mionzi sababu pia zinatumika kama antena ya simu, 4.Usiweke simu kwenye Mfuko wa suruari au shati au kiunoni,sehemu za mwili zinapitisha mionzi vizuri zaidi sababu pia ni njia ya neva za ubongo na chini ya mwili. 5.Usitumie simu kwenye chumba kidogo au lift au gari. Sababu Simu itatumia nguvu nyingi kuvuta mionzi ili kuwezesha mawasiliano. 6.Ukipiga simu subiri hadi mtu apokee ndipo uweke sikioni kusikiliza na sio wakati ina connect. 7.Usipige simu kama network ipo chini au signal inaonyesha bar moja au ndogo, simu itavuta mionzi zaidi ili kufanya mawasiliano 8.Ukinunua simu hakikisha unasoma kama ina LOW SAR (Specific Absorbtion Rate) Ni kipimo cha kupokea mionzi ya simu Za nokia zinazo ila za Kichina HAZINA. 9.Tumia vifaa vya kupunguza Mionzi vinapatikana madukani (vinawakawaka taa hivi) 10.Weka simu atleast 3.4 inches kutoka kwenye sikio 11.Jitahidi kutumia Earphones muda wote unapotumia simu 12.Tumia speaker phone."Loudspeaker " 13.Text zaidi kuliko kupiga simu . 14.Jitahidi usitumie muda mwingi kwenye simu kama umeiweka kwenye sikio 15.Jitahid kuiweka mbali na reproduction organs zako hasa kwa wanaume ambao hatujapata watoto.

SIMU ZA MKONONI NA KANSA YA UBONGO: BALAA JINGINE KWA AFRIKA?

Kwa muda mrefu kumekuwa na mjadala mkali kuhusu nguvu za mionzi ya mnunurisho inayotolewa na simu za mkononi kama zinaweza kusababisha kansa ya ubongo ama la. Hatimaye Shirika la Afya Duniani limetoa tamko kuhusu utafiti unaoonyesha kwamba simu za mkononi zinaweza kuwa zinasababisha kansa ya ubongo. Hatari hii inasemekana kuwa ni kubwa zaidi kwa watoto wadogo na matineja kwani mafuvu yao bado hayajakomaa sawasawa. Naomba hii isiwe kweli kwani kama tunavyojua, Afrika ndiyo jalala la bidhaa feki, mbovu na zilizoisha muda wake. Bila shaka nitakuwa sahihi nikisema kwamba simu zinazotoa mionzi hatarishi kwa binadamu na zitakazokuwa zimepigwa marufuku sehemu zingine za dunia ndizo zitarundikana Afrika. Kama utafiti huu ni wa kweli basi miongo kadhaa tu ijayo Afrika itakumbwa na mripuko wa kansa ya ubongo – mojawapo ya kansa hatari kabisa na inayohitaji tiba ghali sana! Tunachoweza kufanya kwa sasa ni kufuata mapendekezo yaliyotolewa yakiwemo kununua simu zisizotoa mionzi mikali zaidi, kuweka simu mbali na sikio wakati wa maongezi na kwa wenye uwezo kununua vifaa vinavyosafirisha mawimbi ya sauti kama “Bluetooth”. Vifaa hivi huwekwa sikioni na vinaweza kudaka mawimbi ya sauti ya simu iliyowekwa mfukoni au sehemu nyingine na kuyasafirisha sikioni kwa msikilizaji bila madhara yo yote.

Monday, 17 September 2012

Elinaja kijana aliyeamua kuandika bongo fleva kwenye mtihania atoa single yake mpya akimshirikisha barnaba.


Bado Tanzania haijamsahau huyu mwanafunzi ambae aliongelewa sana wakati matokeo ya form IV yalipotoka mwaka jana kutokana na kuandika mistari ya bongofleva kwenye mtihani wake baada ya kuona hakuna chochote alichopata kwenye elimu.
Elinaja alisema  aliamua kuandika mistari ya bongofleva ili wahusika wapate msg, hata hivyo alisema kitu ambacho ana uhakika uwezo wa kukifanya anao ni muziki ambapo amerekodi upya single yake ya Mr President na kumshirikisha Barnaba, bonyeza play hapo chini kumsikiliza na kudownload.

Monday, 10 September 2012

Faida za Tende Mwilini Mwako.

Je unajua kwamba tende ndio tunda pekee lenye kuupatia mwili vitu vinne kwa wakati mmoja, vitamin,protini,wanga na mafuta?. Mbali na utamu wake tende ambazo hulika sana Mwezi wa Ramadhan zina faida nyingi sana kwa mwili wa binadamu. Ebu zijue faida zake……. Tende ni tunda ambalo linayeyuka kirahisi tumboni, na lenye faida nyingi sana ambazo hulifanya liwe tunda la kipekee. Baadhi ya faida zake mwilini ni kama ifuatavyo: 1-Kwa watu wenye matatizo ya tumbo, nicotinic inayopatikana kwenye tende,husaidia kurekebisha matatizo ya tumbo na huleta ahueni kwa watu wenye matatizo ya kupata choo. 2-Tende husaidia kuuimarisha moyo. Iloweke tende kwenye maji kwa usiku mmoja na asubuhi kunywa maji hayo pamoja na tende zilizolewekwa baada ya kuondoa mbegu,ukifanya hivyo mara mbili kwa wiki,moyo wako utakuwa imara. 3-Tende husaidia pia kwenye mambo ya malavi davi. Iloweke tende kwenye maziwa ya mbuzi usiku, asubuhi changanya maziwa hayo na asali,kisha kunywa, njia hii husaidia kuongeza nguvu na stamina za kufanya mapenzi. 4-Utafiti umeonyesha kuwa tende husaidia kutanua misuli ya mji wa mimba,wakati mwanamke anapokaribia kujifungua,hii husaidia kumfanya mwanamke asipoteze damu nyingi wakati wa kujifungua. 5-Wataalamu wa vyakula, wanazichukulia tende kama chakula bora kwa wanawake wanaonyonyesha,kwani husaidia kuyapa maziwa virutubisho muhimu vinavyomfanya mtoto awe na afya njema. 6-Tende husaidia kupunguza kiwango cha kilevi (alcohol) kwenye damu. Maji ya kunywa ambayo tende imelowekwa ndani yake husaidia kuondoa haraka alcohol mwilini. 7-Tende husaidia kuchelewesha dalili za uzee,na pia husaidia kurekebisha ngozi na huondoa mabaka ya kuungua na jua. 8-Kutokana na madini ya chuma kwenye tende,watu wenye upungufu wa damu hupata ahueni. 9-Vitamin B1 na B2 zilizopo kwenye tende,husaidia kuyapa nguvu maini. 10-Tende pia huleta ahueni kwa watu wenye kikohozi na mafua.

Tuesday, 21 August 2012

BARUA KWA VIVIAN TILLYA FROM teamSUA-HIP HOP



 Dear Vivi....


Ni miaka saba sasa tangu uondoke na tunakukumbuka sana michano yako na mambo mengine mengi....(jalini ubinadamu msifanye mavitu kama sanamu.....). Natumai umeonana na Faza Nelly,DOG Nacko.Papaa,Mlost na Pacha Izzy na wengine wengi waliokuja huko.

Dhumuni la barua hii ni kukusalimu na kukujulisha yanayoendelea Arusha.
Mengi yametokea ila ya Muhimu kukufahamisha kuhusu harakati za Muziki hapa Arusha.
Imagine eti siku hizi Metropole,Ricks,Mawingu na Crystal club hazipo tena.
Machizi wengi wamehamia Dar es salaam(just like you...) ila wao wamebadilisha hadi majina wanakuja Arusha kufanya show na kusepaz.
Machalii wapya kibao kwenye Game na wanakalisha usipime wengine wako mbele na wanafanya harakati zilezile Kzz wa X plastaz hajarudi bado tangu aende na anatoa Mixtape moja kali sana hivi karibuni,Chindo pia anawakilisha akiwa huko si unajua tena Jamaa alivyo mbishi.
Jcb na Spark bado ni hardcore(...wana makid asee).

maprodyuza wengi wapya na Studio nyingi.WATENGWA kuna Daz Naledge,DX amekuja na Noizmeka,hata Ngalimi siku izi kuna Studio asee KZ kaja na KAZAWAZA.Grandmaster siku izi wanapiga mpaka VIDEO bana.zipo mingi siwez hata kuzitaja zote.

Harakati zote zile za rap sasa hivi zimeamia Kijenge ya Juu(S.U.A Free-Stage

Watu kibao wanakutana na kupiga freestyle,michano na magrafiit kibao.

Si unakumbuka vile ulikua ukikasirika kuona hakuna mademu kwenye HIPHOP concert na ukawa unaamua kuonyesha uwezo wako dah! ulikua unakalisha asee(.....sa nani wakuongoza safari wote tunaujua usukani.......siwaelewi! )
Juzi si kuna madem wakaibuka SUA bana asee tulikukumbuka sana laiti ungekuwepo ungefarijika kinyama.

Kuna redio stesheni mingi niaje! karibu kila mtaa na maclub za kutosha huko town usiku kama tu mchana. ... kuna masista Dread wengi peace kama wewe.... inapendeza

Arif mambo kibao yamebadilika... kutoka TAPE na disc man siku izi kuna mavitu yanaitwa I-pod,I phone na ma-I pad kitu touch screen maamaaa si unajua Swagga tena...(sorry i know you now know about Apples kama sio matunda tena nikikuambia mambo ya Blackberry si ndo utadata kabisa...hahahahaha!!)

I will tell you about it next time sahivi naenda misele so kama vipi mpe hi Complex(Mwambie alivyosepa tu BTOWN CLAN wakaNYAMAZA ooh SH**T MIKOSI WAMENYAMAZA.....),James Dandu,Drob,Steve2k,produza Roy na wengine mlioko nao huko.

Jumapili tarehe 26 SUA itakua ni spesho kwako na Complex wa2 watapiga mistari yenu..oooyyyy! .Nitakujulisha zaidi next time.

Wako Wapendwa
Katika HIP HOP
###teamSUA###


VIVIAN TILYA  ALIFARIKI DUNIA 21AUGUST KWA AJALI YA GARI ILIYOTOKEA MBWEWE AKIWA NA COMPLEX.

UNAKUMBUKWA NA FAMILIA YAKO NDUGU JAMAA NA MARAFIKI.

NAAMINI UMEKUTANA  NA FREDY JEBI, FATHER NELLY, MLOST NA PACHA ONE.

TUTAZIDI KUWAKUMBUKA..BWANA ALITOA NA BWANA ALITWA UPUMZIKE KWA AMANI VIVIAN.
AMENI.........



Saturday, 11 August 2012

Exclusive: Makala ya kusisimua kuhusiana na maisha magumu ya mdogo wake Obama



Obama's slumdog brother: Kutana na mlevi asiye na matumaini aishie jijini Nairobi ambaye ni mdogo wake na rais wa Marekani


Makala hii imetafsiriwa kutoka kwenye gazeti la Daily Mail mwandishi akiwa  ANDREW MALONE. Makala hii imechapishwa jana, August 10, 2012.

Wakati mwanaume mrefu na anayejulikana sana akiondoka kwenye kibanda chake kilichopo kwenye makazi fukara kabisa barani Afrika wiki hii, baadhi ya watu walianza kumuita kwa utani:‘Mister President! Mister President!’

Akielekea kupata kifungua kinywa huku akivuka mifereji inayotiririsha maji machafu, muonekano wa jamaa huyu mrefu na aliyekonda, unavutia vicheko vya chini chini kutoka kwa watoto wanaocheza kwenye jalala.

              George akiwa kwenye nyumba anayoishi

Jina la jamaa huyu ni George Hussein Obama, ni mdogo wake na Barack Hussein Obama, rais wa kwanza mweusi wa Marekani na mwanaume anayeheshimika zaidi duniani.





Wanaume hawa wawili wanachangia baba lakini Barack Obama alizaliwa Hawaii kwa mke wa pili wa baba yao ambaye ni mmarekani na George alizaliwa nchini Kenya akiwa mtoto wa mke wanne wa mzee huyo.

Leo, wakati Barack akifurahia maisha kwenye Ikulu ya White House, akiruka kwenda nje na Air Force One na ni rafiki wa mastaa wa filamu na wengine mashuhuri, George, 30, anapatikana akiwa amechoka kwenye makazi yake ambayo hata wakazi wenzake wa eneo hilo maskini jijini Nairobi wanayaona kama kichuguu.




Ingawa anadai kutotumia heroin au cocaine, George hutumia muda mwingi kunywa Gongo (Chang’aa) kuanzia anapoamka mpaka muda ambao huanguka na kuzima kabisa.

Gongo anayokunywa ni ile iliyochanganywa na kemikali ya ethanol, na kuongezea acid kutoka kwenye betri ili kuipa kick zaidi, na mchanganyiko huu husababisha upofu na kifo inapochanganywa vibaya.

Kiasi kidogo tu cha pombe hiyo huwafanya hata wanywaji wazoefu kulewa kiasi cha kushindwa hata kukumbuka majina yao. Wanywaji wa mara kwa mara huathrika maini na figo ama ubongo.


Nilipomtafuta George asubuhi siku moja kufahamu maisha yake, alikuwa tayari kwenye kibanda kimoja jirani akinywa Chang’aa ambapo ngono na machangudoa ni sehemu ya menu na hufanyika kwenye kitanda kilichowekwa nyuma.

Utambulisho unafanywa na ‘mpambe’ wa George  — mkazi wa eneo hilo mwenye macho mekundu na mnywaji mwenzie ambaye anamvuta George nje ya kibanda hicho na kumwabia aje kumuona mzungu nje (shouting at him to come and see the ‘muzungu’ (white man) outside.

Baadaye baada ya kusalimia, ninafanya kosa. Namkaribisha George kwaajili ya chakula cha mchana kwenye hoteli yangu. Kwa siku mbili zilizofuatia, aliivamia baa yangu ndogo, kuwaalika wapenzi wake kibao na washkaji zake kula na kunywa kwa gharama zangu na kujionesha kama staa aliyeharibikiwa.

Aliomba pia ‘kitu kidogo’ — Swahili for something small, which, of course, means something large and financial — na alichukia baada ya mimi kukataa kuwapa hela mademu zake.

George pia aliendelea kulaumu kuhusu jina la Obama kuwa kama mzigo na laana kwake, ilhali wakati mwingine bila aibu hulitumia jina hilo kupata hela nyingi iwezekanavyo ili kuzitumia kunywa na kuvuta bangi.

‘Watu wanavutiwa na mimi kwasababu ya kaka yangu,’ anashusha pumzi na kushusha  Johnnie Walker mbili kwa mpigo. ‘Nachukia’. Watu wanapenda niwe mtu mwingine.’

Mara ya kwanza George alikutana na kaka yake alipokuwa shule ya msingi. Barack alienda Nairobi miake michache tu baada ya baba yao kufariki kwa ajali ya gari. George anakumbuka alikuwa akicheza soka wakati kaka yake alipowasili kumsalimia.

Mara ya pili wanakutana ni kipindi Obama — alipokuwa Senator na alifanya ziara ya Afrika Mashariki mwaka 2006, na kutembelea Nairobi kuiona familia yake.


George anasema kwa sasa watu wanamshinikiza afuate nyayo za kaka yake kwenye siasa. ‘Nina watu wengi ambao huniambia nigombee ubunge. Lakini sivutiwi na siasa.’

Kisha anatulia, na kuongeza: ‘Lakini kama Barack angekuwa rais na mimi ningekuwa rais wa Kenya ingekuwa rahisi kuonana.’

Anasema umaskini wake ndio unawazuia ndugu hao kuwa na uhusiano wa karibu.


‘Ana majukumu. Hatakiwi kunilea mimi,’ anasema. Mimi ni mtu mzima, kila mtu hudhani kuwa huwa ananitumia fedha. Lakini mimi sio ombaomba.’ Lakini alipoulizwa iwapo aatachukua fedha akipewa na Obama alisema: ‘Seriously! Yes! Who wouldn’t?’

George alikulia jijini Nairobi akiwa na mama yake ambaye aliolewa tena na mfaransa aliyekuwa anafanya kazi kwenye shirika la misaada jambo ambalo anadai lilimfanya awe hivyo.

Alianza kunywa pombe na kuvuta bangi akiwa na miaka kumi, miaka mitano baadaye alifukuzwa kwenye shule ya boarding, ambako alicheza rugby na kujifunza lugha za kigeni kutokana na kutumia madawa ya kulevya.

Anakubali kuwa alikuja kuwa addicted na cocaine na heroin akiwa na miaka 17, na kuwa mwizi wa kutumia silaha ili kupata hela ya kunywea pombe.

Mwaka 2003 alifungwa jela kwa kosa la kuiba kwa kutumia silaha.

Alikaa kwa miezi tisa kabla ya kutoka kutokana na kukosekana ushahidi.

Swali ni je! George anastahili kuishi maisha haya wakati kaka yake ni rais wa Marekani?

Friday, 10 August 2012

LINEX AOMBA RADHI WANAWAKE WOTE NA JAMII KWA UJUMLA





siku chache baada ya msanii Linex kutoa video ya wimbo wake (AIFOLA), ameandika katika ukurasa wake wa facebook, akiomba radhi kwa wanawake wote kutokana na kipande cha video yake ikimuanyesha akimpiga kofi mschana aliekuwa anaigiza nae katika video hiyo kutokana na kupata malalamiko mengi yanayodai kuichochoa jamii katika vitendo hivyo hasa kwa wanaume

"Naomba radhi kwa kila mwanamke Dunian kofi nililompiga vdeo gal wa kwenye aifola vdeo sikua nakusudia uchochezi wa mwanamke kupigwa na mwanaume wake natumai wanaume wenzangu mmenielewa lengo ilikua kutafuta uhalisia wa matukio kwenye vdeo yangu #team mwanamke hapigwi analiwazwa na kubembelezwa..." amesema linex




KUTOKA KWENYE MUZIKI HADI TV,DRAMA INAYOITWA FX



Dr.Dre ni kati ya wasanii wa Hip Hop waliopata heshima sana katika game na alitajwa katika marapper watano wenye mkwanja akiwemo P.Diddy, Jay Z, Birdman, 50 cent na yeye mwenyewe Dr Dre. Katika mauzo ya headphones zinazofahamika kama beats by dre zilimumrudisha Dre hadi juu na kuwa kati ya marapper wenye mkwanja, Na kwa sasa yuko tayari kuanza kuonekana kwenye Tv Drama mpaka sasa bado anaendelea kumalizia script ya Drama FX.

SINTA:HUYU NI NANI?ETI MUIMBAJI?HAPATIKANI HATA GOOGLE AU NDIO WALE KIINGILIO BUKU UZINDUZI TANDALE





leo hii katika pita pita zangu, nimekutana na story hii iliyoandikwa kupitia sintah.com, ikionekana kuwa ni majibu kwa Ney wa mitego, baada ya kuongea kwenye Take one kuhusu single yake ya NASEMA NAO na kumtaja mwanadashosti Sintah kuwa anafanya chochote kile ilimradi arudi kwenye game...... na haya ndio majibu yaliyofumuka.....
hivi wa wapi weweee,mbona husomeki weweee,tume google
hupatikani wewe,shukurani kwa mdogo wako alietuletea picha yako ya beach, sijui nani sijui nay utaweza??
jipange,namuonea huruma mama yako kuzaa kiumbe
kilichoharibikiwa, nina jaribu ku google naona neyo wa Us sasa nisaidie nitupie kwa mnyamani au kiembe mbuzi niambieeee ili nikupate my brodaaaaa you have just tickled a private part of a tiger,,, you wanted promo now you gotta maza vitumbua 
NEY WA KUJITEGA MWENYEWE MAANA
UNA CHASTE  MBU SIJUI UTAMTEGA NANI, KAMA UNA SHIDA NA MIMI DJ DJ DJ AND MY BRODAA CHOKA ANAJUA NINAPOEGESHA MILONJO YANGU  SASA KAMA UNATAKA KUIKATA KAMA ULIVYOWAMBIA WATU WAKO BBM(MAANA HU HUNA HADHI YA KUKAA KTK MY BBM LIST) MWAMBIE AKULETE MDOMO HUPONZA KICHWA NA UMEJIPONZA LOVES LEO NIMEWAFUNGULIA COMMENT MTU AKIGUSWA ATAJIJUA MAANA NIMECHOKA KUONEA WATU HURUMA KAMA NOMA NA IWE NOMA
NEY NIMESHAMPA RUHUSA MLINZI AKURUHUSU UINGIE SWALI ANAKUJUA??? JIPANGE ULIPOCHOKOZA SIPO KABISA UNSTOPPABLE NOTHING BUT CONFIDENCE
MSICHANA AMBAYE ANA TWO SIDES (COOPERATE FIGURE NA ACTRESS) OOH SORRY USIJE MCHANA NITAKUWA SERENA NINA APPOINTMENT NA WORLD BANK CREW CONCERNING MY LAUNCH  

SINA SHIDA NA  MTU ILA UKINIANZA HUWA NAMALIZA  SHIDA ZAKO 
cc to naxylady upo kwenye cue usitafute maarufu maana umaarufu hauji kwa njia za panya from Unstoppable
MA International Relations & Diplomacy

Saturday, 28 April 2012

AJALI YA BASI LA COAST LINE



Hili ni basi la Coast line ambalo limepata ajali siku ya leo Juma mosi asubuhi katika kijiji cha Terrat kilichopo wilayani Sianjiro Mkoani Manyara.


Basi hilo lilikuwa likitokea Mkoani Arusha likieleke Mkoania Dodoma,na ndipo lilipopata na ajali hiyo katika eneo la kijiji hicho baaada ya STALING kukatika na kusababaisha kuugonga mti uliokuwa kando ya bara bara hiyo na kupelea tairi za mbele zote 2 kupasuka.


Basi hilo limeharibika vibaya sehemu ya mbele upande kulia ambao huwa anakuwa Dreva,amabaye amevunjika mguu mara mbili na abiria wengine kupata majeraha mbali mbali.



           Hawa ni baadhi ya abiria walionusurika katika Ajali hiyo



Na huu ndio mti wa Mgunga ambao Basi hili la COAST LIME limeugonga baada ya Kukatika STALING.

By Kiwa Strong..

Wednesday, 25 April 2012

KWA NINI VIUMBE WENGI WANA MACHO MAWILI

Nilikuwa natafakari juu ya uumbaji na kushangazwa na kitu kimoja cha ajabu; viumbe vingi hata vinavyoishi mazingira tofauti na vya aina (specie) tofauti sana vimefanana kwa kuwa na macho.


Vinaweza vyote visiwe na miguu, mbawa, au pua lakini karibu vyote vina macho. Kuanzia majini, angani na nchi kavu viumbe vingi vinamacho! Wadudu wadogo na wanyama wakubwa wote wana macho; samaki na ndege hadi minyoo ina macho! 

Na katika maajabu ndani ya maajabu ni kuwa viumbe vingi vina macho mawili (sijajua kama yupo mwenye jicho moja) na vile vingine vina macho mengi (compound eyes). Angalia mifano hii:

Angalia Nyoka:




Angalia Samaki:




Angalia Ndege:


Angalia Vipepeo


 


Angalia Mchwa





Angalia Nyangumi


Angalia Kaa:



Angali Nyani:




Kwanini?
Jibu la kisayansi ambalo hutolewa mara nyingi ni "evolution"; lakini kwanini "eyes"? Utaona viumbe vinafanana vitu vingi tu lakini mara nyingi tofauti ni idadi.


kwa mfano viumbe vingi vina miguu minne (wanyama) lakini vipo vyenye miguu sita (wadudu) na vingine havina miguu kabisa (nyoka na samaki); lakini vyote vina macho! Kwanini macho ni mojawapo ya viungo ambavyo vinaonekana karibu katika viumbe vingi zaidi kuliko viungo vingine? Na kwanini mara karibu zote macho hayo yanakuwa mawili siyo matatu au manne (kuangalia pembeni, juu na chini)? 

Monday, 23 April 2012

NJIA KUMI KUSAIDIA KUPUNGUZA UNENE..

Kati ya sababu kuu zinazopunguza uhai wetu ni afya, unene na kutojua kujiangalia vyema.

 
1-ULAJI
Ipo mifumo miwili ya kula. Chakula unachokula na namna unavyokila.
Unavyokula.

Kuna kula vyakula vidogo vidogo vyenye madini, vitamini, mafuta nk mara nyingi kwa siku; au kula milo michache (mmoja au miwili) mikubwa ili kujaza tumbo. Ulaji mdogo mdogo husaidia afya na kuingia mwilini vyema kuliko ulaji mkubwa wa mara chache.

Tumbo lina musuli zinazofanya kazi kama mashine au mnyama. Gari likijaa sana hupata taabu kwenda. Punda hivyo hivyo. Ulaji mdogo mdogo unaosambazwa mara kadhaa kwa siku  ni bora maana mwili unachambua kila kitu kwa wepesi na haraka. Unapokula milo michache mikubwa unapalilia zaidi mafuta mwili.

(PENDEKEZO la kwanza.  Asubuhi, kunywa maji kwanza, matunda, kisha ndiyo chai na vitu vingine kama mkate au maandazi…)

Wapo wanaodai kwamba wanakula matunda na mboga...

Tatizo ni kwamba mipangilio  yao huwa ya makosa. Mathalan wengi hula matunda baada ya chakula. Vimeng’enya  chakula (enzymes) tumboni hufanya kazi namna tofauti. Mathalan vile vinavyonyambua matunda ni tofauti na vinavyomeng’enya vitu vigumu zaidi kama nyama au wanga.

Matunda hunyambuliwa haraka zaidi kuliko vyakula vingine. Hivyo ni bora kula matunda dakika10-20 kabla ya chakula. Ukila baadaye matunda hugeuzwa aina fulani ya pombe (fermented food) inayoelea tu juu ya chakula na kubakia kitu kingine badala ya kuingizwa haraka ndani ya damu kupitia utumbo mdogo, uwengu, moyo, ini, nk.

Tatizo jingine ni kupika sana mboga hadi zikapoteza nguvu.

Mseto wa vyakula pia ni muhimu. Kwa mfano vyakula vyenye uchachu (acid) na vile vinavyomumunyuka haraka (alkine) havitakiwi viliwe pamoja. Mfano ni matunda.

Matunda chachu kama machungwa, mananasi na maembe yatakiwa yawe pamoja; na yale laini zaidi:  ndizi mbivu, matikiti maji, mapapai, matufaha, nk yaende kivyake, maana yana mfumo tofauti, wa kumeng’enywa.

 

Chakula unachokula.....

Waafrika  hatuna tabia ya kula mboga mboga mbichi. Tunafuata ladha na mazoea kuliko thamani.
Bara letu lina mboga na vyakula bora kuliko bara lolote duniani lakini sisi tunakufa mapema na kwa utapia mlo kuliko wale wanaotoka nchi kame.

Ulaya nzima imejazana mboga mboga zinazoagizwa toka Afrika. Kenya na Tanzania zinauza mboga za maharagwe mabichi (green beans), matunda toka Afrika Kusini na Ivory Coast; nk. Waafrika tunapenda kujaza matumbo. Unene umekithiri hata wale walio matajiri waliosoma bado wanakufa kwa kisukari shauri ya kutokula mboga mbichi.

Ulaji wa mboga mbichi ni upi?

Ni mathalani ulaji wa salad. Tanzania tunaita kachumbari. Lakini si lazima iwe kachumbari ya nyanya, vitunguu na chumvi tu. Waweza kuchanganya matango, nyanya kwa maparachichi; au vitunguu saumu, giligilani na karote.

Huu mseto wa mboga mbichi ni mzuri ukienda na chakula chenye nyama za minofu na wanga (ugali, wali, ndizi za kupika nk). Ulaji wa wanga asubuhi, mchana na jioni kila siku huchangia sana katika unene.

2-UNYWAJI  MAJI
Waafrika hatunywi maji, hasa wanawake. Wanaokunywa maji zaidi ni wacheza michezo. Wengi wetu hunywa zaidi soda (vinywaji baridi kama Cocacola, Pepsi, Mirinda ,Tangawizi  na gesi za kisasa kama Red Bull) zilizojaa gesi inayoleta vidonda tumboni; na chai.

Kuliko maji. Na maji haya hutakiwa  dakika 10-20 kabla ya chakula au nusu saa kuendelea baada ya chakula. Ukila  chakula huku unasakatia maji huimanisha mtu una kiu.

Ulaji chakula na unywaji maji ni vitu viwili tofauti. Ila utawaona watu wanakula huku wakibugia maji. Unapokula chakula huku unabugia maji unapunguza nguvu za chakula, unajaza tumbo maji na kuchelewesha mmeng’enyo wa chakula (digestion).

Chakula kisipomeng’enywa vizuri kinaketi tu tumboni. Matokeo wengi wetu tuna  matumbo makubwa. Kama hufanyi mazoezi lile tumbo linakwenda pembeni (chini ya mbavu) hasa kwa watu wa makamo linaleta maradhi kama kisukari, kiungulia, kuvimbiwa, uyabisi wa tumbo, nk.


3-SUALA LA UMENG’ENYAJI

Chakula huanza kumeng’enywa au kusagwa (kwa lugha iliyozoeleka) mdomoni. Mate yako mdomoni ni chanzo cha uchambuaji chakula. Unapobugia chakula bila kutafuna sawasawa unasababisha mambo mawili.

Moja chakula kutochambuliwa vizuri, pili chakula kwenda kukaa tu tumboni, au kama kikipita hakisaidii lolote mwilini.

Utafunaji wa taratibu husaidia umeng’enyaji. Chakula kinapofika tumboni hukaa pale dakika ishirini. Hapo huchanganywa na asidi (ya manjano iitwayo Hydrochloric) inayokibadilisha tayari kupelekwa utumbo mkubwa, kupitia kongosho.

Kule uchafu utapelekwa chini na rutuba kusafirishwa na utumbo mdogo kuelekea katika uwengu, moyo. Moyo utadunda chakula kilichoshageuzwa damu kuelekea mwilini kufanya kazi na akiba hubakishwa katika ini.

Sasa kama usipotafuna vizuri, ukila huku unakunywa sana maji au vinywaji vingine chakula hakimeng’enywi vizuri. Ndiyo maana unawaona watu wengine wanakula sana lakini hawana afya.

Wanaugua ovyo ovyo, wanatoka jasho ovyo, wanajamba ovyo, wana matumbo makubwa, wanavimbiwa, wanakaa siku nyingi bila kwenda choo (inatakiwa mtu kwenda haja kubwa mara moja au mbili kwa siku) nk.

Misitu na hewa safi ya mimea

4-ULAJI WA VYAKULA VYA MAFUTA

Mafuta ni suala muhimu sana mwilini. Ila ulaji wake shurti uwe wa mpangilio. Yaani unaowiana. Lazima mtu uwe na wastani mzuri wa vyakula vya nguvu, yaani “wanga” (ugali, ndizi, wali, viazi mbalimbali, mikate, mahindi, nk), ujenzi yaani “protini” (mboga na nyama), “madini” (mbegu mbegu mbichi si za kukaanga sana na chumvi) na “vitamini” (matunda, maziwa, mayai, nk).

Waafrika tunapenda nyama. Nyama ni muhimu sana maana ina madini aina ya chuma (nyama nyekundu) protini,nguvu na mafuta. Ila mafuta yaliyoko katika nyama mara nyingi si mazuri shauri hayatoki, huganda.

Chukua nyama ya kuku na samaki ambayo huwa na ngozi. Wengi wetu hupenda sana kula ile ngozi ya wanyama hawa kwa kuwa tamu. Lakini haya ni mafuta mabaya.

Mafuta ya samaki lakini ni mazuri. Samaki anayo mafuta ya Omega-3 ambayo husaidia mwili na kinga maradhi mwilini.

Tunapokula nyama choma au ya kukaanga, lazima tule pia mboga za majani (mbichi) na si vizuri kula nyama kila siku. Kama huwezi kukaa bila nyama kila siku, fanya mazoezi ya mwili.

PENDEKEZO LA 3- Kula mbegu mbegu za korosho, karanga au mlozi (ziwe mbichi badala ya kukaanga na chumvi) kati kati ya siku. Haya ni mafuta yenye rutuba mwilini kuliko nyama za mafuta.


Chips za Magimbi

MAZOEZI YA MWILI NA VIUNGO

Mazoezi ni mfalme wa kupunguza unene.

Ukiwauliza wengi watakuambia wanafanya kazi ngumu za sulubu (wanachuruzikwa jasho) kwa hiyo hayo ni mazoezi. Ila kazi na mazoezi ni vitu viwili tofauti. Ingekuwa kufanya kazi ni mazoezi basi kusingekuwa na wastani mfupi wa maisha kwa maskini hasa sisi Waafrika.

Wengine watadai kwamba walipokuwa wadogo shuleni walifanya mazoezi sasa wamekuwa watu wazima (miaka 40 kuendelea) kwamba eti mazoezi ni suala la ujana; kumbe kadri unavyokuwa ki umri ndivyo kadri unavyotakiwa kufanya mazoezi na kujitazama zaidi kiafya.

Watazame Wachina na Wajapani wanavyoishi maisha marefu.

Mazoezi ni shughuli inayokufanya kwanza uheme (mapafu na moyo kwenda kasi), viungo na mifupa kujinyoosha (stretching), kutoka jasho na usafishaji wa damu.

Mazoezi yanayosaidia haya ni pamoja na kutembea kasi, kukimbia, kuogelea, michezo mbalimbali ya riadha (kama mpira wa miguu, nyavu, kikapu, mikono, nk); michezo ya kupigana na kujilinda yaani masho ati(karate, kung fu, judo, capoeira, krav maga, jiu jitsu, systema, kickboxing, thai boxing, kempo, kalari payatu, aikido, nk)

Ni muhimu mwanadamu ufanye mazoezi makali ya viungo mara mbili tatu kwa juma. Si vizuri kufanya kila siku kwani musuli na mishipa inahitaji kupumzika na kukua.

Kama unapenda kuinua vyuma lazima uwe na mwalimu wa kukuelekeza; na si vizuri kufanya kila siku.  Wastani wa mara mbili tatu kwa juma inatosha kabisa.

 

6-UPO UFANYAJI MAZOEZI WA AINA MBILI

Mazoezi ya nguvu ya kuhema niliyotaja hapo juu (cardio-vascular) na yale laini ya kujinyoosha yaani ambayo hutumia zaidi nguvu za ndani na pumzi.

Haya ya pili ni kama Yoga (India) , Tai Chi Chuan (China) na aina mpya mazoezi iliyoanza Majuu miaka ya karibuni yaani Pilates (hutamkwa hivyo hivyo ilivyoandikwa Pilates).

Haya laini yanawafaa zaidi watu wazima na nchini China na Japan mathalan utawakuta wazee wa miaka 80 hadi 90 bado wanayafanya. Husaidia moyo, damu na akili.

Michezo na mazoezi ya mwili ni njia kuu ya kupunguza unene, kurefusha maisha, kuchangamsha ubongo, kupunguza ulevi, uvutaji sigara, dawa za kulevya, tabia mbaya za uvivu, ugomvi, nk.  Mataifa yenye watu wanaofanya mazoezi kama Japan, Brazili, India, China nk  huwa na wachapa kazi wengi na wananchi wanaoipenda jamii yao.

Chakula cha wanga kwa wingi kilichozoeleka sana Afrika ni kitamu; ila kinakosa mboga mbichi za majani, yaani Saladi

7-KULA SANA CHUMVI SI VIZURI

Ulaji chumvi mwingi hutokana na suala la ladha. Kisayansi vyakula  vyote vina chumvi asilia sema tu tumezoea kuongezea madini hii iitwayo Sodium.

Sodium inachangia sana kufupisha maisha. Huifanya mishipa ya damu ichoke; ni kama bomba lolote la maji ukilitazama baadaye hugeuka rangi kutokana na yale maji kupita pale kila siku.

Kwa wale tunaoishi nchi za joto na kutoka sana jasho kula chumvi ni muhimu. Ila tatizo letu ni kwamba hatunywi maji ya kutosha.

Mtu ukiwa na kiu unakunywa soda au kinywaji cha sukari; inakuwa kama unaendelea kuutesa mwili.

Kwa vipi? Mishipa inayopitisha damu mwilini badala ya kusaidiwa kwa maji inawekewa kazi zaidi ya kusafisha sukari na chumvi. Ndiyo maana vifo vingi vinatokea mapema; wastani wetu wa maisha haupiti miaka 50.

Utafiti uliofanywa chuo kikuu cha California, Marekani mwanzoni mwa 2010, umethitibisha kwamba vifo vingi duniani husababishwa na maradhi ya moyo na saratani ambavyo hutokana na uvutaji sigara, unene, ulevi na ulaji sana wa chumvi na sukari.
Tukipunguza ulaji wa chumvi tunasaidia pia kupunguza maradhi ya moyo, utafiti unasema.


8-TAFITI ZA VYUO KADHAA ULIMWNGUNI KUHUSIANA NA AFYA

Jarida la Kimarekani la sayansi lilieleza kwamba utapunguza ugonjwa wa moyo (ambao husababishwa na unene , wasiwasi na purukshani) kwa asilia mia 42 kama utakula matunda na mboga za majani peke yake kila siku, juu ya msosi wa kawaida.

(PENDEKEZO LA KULA- Na 4- Kula mlo wako. Baada ya saa mbili au tatu, sakatia tunda au matunda; baada ya mlo mwingine, kula sahani ya mseto wa mboga mbichi kama karote na matango. Utaona tofauti ya afya, ngozi, wajihi,usingizi, nk.

Kidesturi tumezoea kunywa chai au soda za sukari sukari na gesi kati kati nya milo badala ya matunda na mboga mbichi za majani).

Utafiti uliofanywa na wanasayansi  chuo kikuu cha South Carolina mwanzo wa mwaka 2010 kuhusu faida za kuogelea.

-Zoezi la kuogelea  lina faida zaidi ya kukimbia au kutembea kwa vile huchanganya mazoezi makali na pumzi, kusaidia mapafu na moyo. Utafiti ulithibitisha kuogelea hupunguza hatari za kifo kwa asili mia hamsini.

-Utafiti wa jarida la chuo cha uganga Ulaya umeeleza (desemba 2009) kwamba kulala nusu saa kila mchana (“nap”) husaidia  kupunguza ugonjwa wa moyo kwa asilimia 37.

-Uchunguzi wa chuo cha michezo cha Hispania mwanzoni mwa 2010 umethibitisha kwamba ukikimbia mara tatu kwa juma (jogging) unaongeza nyege mwilini kwa asili mia 75. Hasa kwa watu wa makamo mnaoanza kupoteza nguvu za urijali.

-Uchunguzi chuo kikuu cha Leeds, Uingereza  mwanzoni mwa 2010 umeonyesha unapotembea kwa miguu, ukikwepa barabara kubwa zisisokuwa na mioshi ya magari (pollution) unapunguza matatizo ya maradhi ya hewa chafu kama pumu, mapafu na appendix.

-Uchunguzi wa chuo kikuu cha Texas mwaka 2010 umegundua kwamba  kula tunda la divai nyekundu mara kwa mara husaidia kupunguza  kupata ugonjwa wa kisukari.

-Hapo hapo tunaelezwa kwamba watu weusi na bara la Asia wanakumbwa zaidi na ugonjwa wa kisukari kutokana na vinywaji vya sukari sukari na gesi (fizzy drinks).

Ukinywa kiasi cha miligramu 300 za vinywaji hivi (Cocacola, Red Bull, Fanta, nk)  kwa siku unajitahadharisha kupata kisukari.

9-KUFUNGA

Neno kufunga linatambuliwa rasmi kuhusiana na Waislamu (mwezi Ramadhani) au Wakristo (Lenti nk). Ufungaji huo una masharti mengine ya kidini tofauti na haya ya kiafya.

Mathalani wafungaji  hawa hula chakula kingi usiku; ukihesabu wanafunga wastani wa saa 12 tu. Kawaida ukitaka virusi na takataka nyingine mwilini zitoweke, au viungo vipumzike wahitaji saa 20 kuendelea.

Ufungaji ninaouongelea ni ufungaji wa kutokula kabisa kwa saa 24, 36 hadi 48 kuendelea…
Ufungaji ni nini?

Kama mashine yeyote mwili wa mwanadamu unahitaji kupumzika na kujisafisha. Hata tukiwa tumelala bado viungo mbalimbali mwilini vinafanya kazi.

Kwa hiyo faida ya kwanza kabisa ya kufunga ni kuupumzisha mwili kama mfanyakazi yeyote anapokwenda likizo.

Faida ya pili ya kufunga ni kusafisha mwili kutokana na uchafu ambao haukutoka (kinyesi hakitoi mabaki yote toka utumbo mkubwa), dawa na takataka za mazingira tunayoyavutia hewa, virusi au kuyanywa katika maji na vyakula mbalimbali na pia uchafu wa hisia, yaani hasira, huzuni, nk.

Kuna ufungaji wa aina mbalimbali.

1-Kufunga kwa kunywa maji tu, saa 24 kuendelea…
2-Kufunga kwa kutokunywa maji au kula chochote, saa 24 kuendelea…
3-Kufunga kwa kula tu matunda au mboga zilizopondwa kama karote, matango nk, saa 24 kuendelea…

Ufungaji huu unatakiwa ufanywe kwa mpangilio. Kitu muhimu si tu kufunga bali NAMNA unavyofungua.

Ukianza kula tena, unaanza taratibu. Kawaida ni vizuri kuanza na maji, kikombe au bilauri ya kwanza taratibu.

Subiri tena nusu saa, bilauri nyingine, halafu hadi ya tatu, halafu ndiyo matunda yasiyo ya chachu, na kadhalika.

Kuanza kufungua kwa kunywa chai ya maziwa, uji au vyakula vingine vya wanga hakusadii sana mfungo huu.

Maana lengo lake ni kusafisha mwili.

10-USINGAJI

Usingaji au masaji ni njia nzuri sana ya kupunguza unene. Ikiwa unaangalia namna unavyokula, unafanya mazoezi na kusingwa mara moja au mbili kwa mwezi unaupalilia mwili vizuri.

Nini faida ya usingaji? Kusinga husaidia ngozi, mishipa ya damu na sura nzima ya mwili na taswira yako mwanadamu.

Wengi wetu tunaposikia neno kusinga tunafikiria usingaji wa mapenzi. Hivi ni vitu viwili tofauti kwani usingaji wa mapenzi unaimanisha mahusiano ya kihisia.

Kifupi mwanadamu unatakiwa uwe unautunza na kuungalia mwili wako kama nyumba au hekalu lako. Wengi wetu tunaoga, tunajipaka marashi, tunasuka, tunanyoa nywele au ndevu; lakini miili yetu kiundani inaoza taratibu…

By kiwa strong...........