Doris
Payne anatuhumiwa kwa wizi wa herini ya thamani ya dola 690, kutoka katika duka
moja la uuzaji wa vitu vya thamani la Saks, katika kiunga kimoja mjini
Atlanta-Marekani.
Wakili
wake anatafuta namna ambayo bibi huyo anaweza kuachiwa huru kwa sababu ya
kudorora kwa afya yake.
Payne
ambaye maisha yake ya wizi yaliwekwa katika filamu mwaka 2013, amewahi kufungwa
jela mara kadhaa kwa makosa mengi tu ya wizi na uhalifu.
Wakuu
nchini Marekani wanasema kuwa ametumia majina 22 ya bandia tangu alipoiba
almasi kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 23, na akaweza kukwepa kutiwa
mbaroni.
Muungano
wa Walinzi wa vitu vya thamani JSA na kampuni moja kubwa ya kibiashara, ilituma
tahadhari kwa maduka yote yanayouza bidhaa na mapambo ya thamani, kujihadhari
na mwizi huyo sugu mapema miaka ya 70.
Rais
wa kampuni hiyo kubwa alitaja tabia ya bi kizee huyo kama wizi au uhalifu wa
aina yake.
Aidha
anastaajabu kuwa angali anaiiba hata akiwa na umri huo mkubwa.
Akihojiwa
na shirika la habari la Associated Press mwaka 2005 akiwa jela, bibi huyo Payne
alisema kuwa haibi kwa sababu ya pesa,ila yeye hujikuta tu akiiba na haoni kama
ataacha tabia hiyo labda baada ya kufa.
0 comments:
Post a Comment