Wataalamu wa masuala ya wanyama
wamegundua kwamba, mamba ana uwezo wa kulala huku jicho lake moja likiwa wazi.
Utafiti
huo ambao umewaacha wengi wakishangaa, kwani picha nyingi duniani huonyesha kuwa
mamba hulala fofofo, wakati jicho lake moja huwa likiona.
Wanasema
hilo hufanyika kwa sababu sehemu moja ya ubongo wa mamba huwa imezima, ilihali
sehemu nyingine ikifanya kazi.
Wanasayansi
wamebainisha kwamba kusinzia kwa jicho moja ni jambo la kawaida kwa baadhi ya
ndege, kama vile pomboo ambao huendelea kuangalia kwa nusu ya ubongo wao ,
wakati nusu nyiongine ya ubongo ikiwa imepumzika .
Utafiti
huo ulichapishwa katika jarida majaribio ya kibaiolojia
0 comments:
Post a Comment