Thursday 1 October 2015

Mbwa atumia wiki tatu kujifunza lugha mpya……

Mbwa aliyekuwa akiandamana na mmiliki wake kwenye darasa la kujifundisha lugha, ameshangaza wengi baada ya kuanza kuelewa lugha hiyo baada ya wiki tatu pekee.

Neil smith alikuwa akiandamana na mbwa wake mwenye umri wa miaka mine kwa jina ginger, akienda kujifunza lugha ya gaelic katika kanisa moja karibu na mji wa dunoon.
Anasema alishangaa kuona jinsi mbwa huyo aina ya English cocker spaniel, alivyoanza kufuata maagizo yaliyotolewa kwa lugha hiyo kama vile keti (suidh), kaa (fuirich), njoo hapa (trobhad) na mbwa mzuri (cu math).
Mwalimu elma mcarthur amesema ginger ni mbwa mwerevu sana.
Bw smith na ginger wamekuwa wakihudhuria darasa hilo katika kanisa la strone church of scotland kila wiki pamoja na watu wengine 23.
Mzee huyo wa miaka 67 alimsifu mbwa wake huyo anayemsaidia kusikia akisema imemuwezesha kujiamini zaidi.

Anasema sasa anafurahia kujionyesha kwa watu wengine na kujivunia kwamba ana mbwa anayefahamu lugha mbili.

0 comments:

Post a Comment