Utafiti mkubwa
na wa kwanza kubaini iwapo umezaji wa tembe za Aspirin kila siku unapunguza kwa
kiwango kikubwa athari ya kurejea kwa saratani umeanza nchini Uingereza.
Jaribio hilo
litahusisha watu 11,000 wanaotibiwa ama waliomaliza matibabu ya aina tofauti za
saratani.
Utafiti huu utakaoendelea kwa kipindi cha hadi miaka 12,
utatathmini matokeo ya kumeza miligram 300 ya Aspirin kila siku na kutofautisha
na kundi lingine litakalokuwa likimeza miligramu 100 ya dawa hiyo.
Makundi hayo mawili yatalinganishwa na kundi la tatu, ambalo
litakuwa likimeza dawa ghushi.
Iwapo utafitu
huu utabaini kuwa kweli Aspirin inapunguza athari ya kurejea kwa maambukizi ya
saratani, basi hii itachochea mwamko mpya katika matibabu ya Saratani ambayo
kwa kawaida hugharimu kiasi kikubwa cha pesa.
Majaribio hayo yataendeshwa katika vituo 100 nchini Uingereza
kwa kipindi cha hadi miaka 12 kuanzia leo.
Hata hivyo onyo limetolewa kuwa, Aspirin haifai kutumika na
kila mtu bila ya ushauri wa daktari.
Hii ni kwa sababu uchunguzi tofauti ulibaini kuwa umezaji wa
dawa hiyo ya Aspirin, husababisha vidonda vya tumbo na pia uvujaji wa damu
akilini, kwa sababu viungo vilivyo kwenye tembe hizo za Aspirin husababisha
damu kuwa maji maji (Nyepesi)
0 comments:
Post a Comment