Filamu
mpya ya Star Wars: The Force Awakens imevunja rekodi Uingereza kwa kuuza tikezi
nyingi zaidi siku ya kwanza ya kuuzwa kwa tiketi.
Tiketi hizo za mapema zilianza
kuuzwa Jumanne, huku filamu hiyo ikitarajiwa kutolewa mara ya kwanza Desemba
17.
Saa 24 za kwanza jumla ya tiketi
200,000 zilikuwa zimeuzwa, na kuvunja rekodi zilizokuwa zimewekwa awali na
Skyfall, Spectre, The Hunger Games na Fifty Shades of Grey.
Nchini Marekani na Canada, Imax
walifichua kwamba walipokea $6.5m (£4.2m) kutoka mauzo ya tiketi.
Pesa hizi ni nyingi mjo
ukilinganisha na mauzo ya filamu za The Dark Knight Rises na Avengers: Age of
Ultron siku ya kwanza, zote ambazo hazikupitisha $1m (£650,000).
"Tiketi zinanunuliwa sana
kote, kuanzia Hollywood na London," alisema afisa mkuu mtendaji wa Imax
Greg Foster.
Filamu ya The Force Awakens ndiyo
ya saba katika msururu wa filamu za Star Wars na imeshirikisha waigizaji kama
vile John Boyega, Daisy Ridley, Harrison Ford, Oscar Isaac na Adam Driver.
0 comments:
Post a Comment