Utafiti
mpya umeonya kuwa sigara ina uwezo wa kuua kijana mmoja kati ya vijana watatu
nchini China.
Hali hiyo itatokea kama
hapatakuwa na hatua yeyote itakayofanyika itakayowafanya waache tabia hiyo.
Utafiti huo uliochapishwa katika
jarida la Lancet linalohusiana na masuala ya tiba, unasema kuwa China
inakabiliwa na ongezeka kubwa la vifo vya mapema, kwa kuwa theluthi mbili ya
vijana nchini humo huanza kuvuta sigara wakiwa chini ya miaka ishirini.
Na karibu nusu hufa kutokana na
tabia zao. Hivyo kama hali ya sasa itaendelea utafiti unaainisha kuwa idadi ya
watu wanaokufa kutokana na matumizi ya tumbaku kila mwaka nchini China
yataongezeka, wengi wao wakiwa ni wanaume ambapo watafikia watu milioni mbili
ifikapo mwaka 2030.
Wanasayansi walifanya tafiti
mbili kwa nchi nzima ndani ya miaka kumi na tano ukiachilia mbali ufuatiliaji
wa athari za kiafya kutokana na uvutaji sigara nchini China.
0 comments:
Post a Comment