Kwa miaka
mingi sasa binadamu amekuwa akitumia pilipili kuongeza ladha kwenye mlo wake.
Sasa
utafiti umeonyesha si ladha tu ambayo pilipili huongeza,bali pia hufanya
wanaoila kuwa na maisha marefu.
Matokeo ya
utafiti yaliyochapishwa kwenye jarida moja la matibabu nchini Uingereza kwa
jina British Medical Journal, yanasema kula mlo uliotiwa viungo, ikiwemo
pilipili, huwa na manufaa kwa afya ya binadamu.
Wanasayanasi
kutoka Uchina waliangazia afya ya watu takriban laki tano waliojitolea
kushirikishwa katika utafiti kuhusu manufaa ya pipili kwa muda wa miaka kadhaa.
Matokeo ya
uchunguzi huo yamebaini kuwa wahusika waliokula chakula kilichokuwa na wingi wa
viungo, mara moja ama mara mbili kwa wiki walipunguza hatari yao ya kufa kwa
asilimia 10.
Viwango vya
hatari ya kufariki pia vilionekana kupungua kwa kiasi kikubwa kwa waliokula
vyakula vilivyotiwa vikolezo kwa wingi kila siku.
Katika
uchunguzi huo sehemu kubwa ya viungo kwenye chakula ilikuwa pilipili, na kwa
waliokula pipili mbichi walionekana kupunguza hatari ya kufariki kutokana na
saratani, ugonjwa wa kisukari na pia maradhi ya moyo.
Hata hivyo tahadhari
imetolewa kwamba vyakula vyenye viungo vikali, haviwezi kuwafaa watu wenye
matatizo ya tumboni kama vile vindonda vya tumbo.
0 comments:
Post a Comment