This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Tuesday, 28 February 2017

WATALII 2 KUPELEKWA MWEZINI 2018...

Safari hiyo itafanyika 2018 kulingana na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya SpaceX Elon Musk, alieongezea kwamba watalii hao tayari wamelipa kiasi fulani cha fedha.

VYOMBO VYA PLASTIKI CHANZO CHA SARATANI….

Imebainika kuwa vifaa vya plastiki hutengenezwa kwa kemikali zaidi ya 200, hivyo kuwa chanzo cha aina 100 za ugonjwa wa saratani.

Monday, 27 February 2017

MAJAJI WAICHARUKIA SERIKALI KESI YA LEMA

Mwenyekiti wa kikao cha jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, kinachoendelea Arusha, Bernard Luanda, leo amegeuka mbogo kwa wanasheria wa serikali kwa kitendo cha kumnyima Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema dhamana kwa lengo la kumyima haki.

WAZIRI KIGWANGALLA AAHIRISHA ‘PRESS CONFERENCE’ YA KUTANGAZA WANAOJIHUSISHA NA USHOGA.

Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangalla, amesema kuwa hawatokuwa na press conference ya kutangaza majina ya mashoga wanaojiuza na kujitangaza mitandaoni.
Waziri huyo aliahidi kutangaza majina na mashoga ambao wanatuhumiwa kujiuza mtandaoni kinyume na sheria.

Jumatatu hii waziri huyo alitoa taarifa ya kuahirisha kutaja majina hayo kwa madai kuna matatizo ya kiufundi.

“Tunaomba radhi hatutokuwa na press conference kuhusu kutangaza majina ya mashoga wanaojiuza mitandaoni kwa sababu za kiufundi!,” alitweet Kingwangala.

Sunday, 26 February 2017

WAVUTAJI MBEYA WALALAMIKA BANGI KUADIMIKA MTAANI (AUDIO)

Wavutaji mkoani Mbeya wamelalamika bangi kuadimika mtaani tangu vita dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya ishike kasi nchi nzima. Mmoja wa wavutaji mashuhuri wa mmea huo ambaye amedai kuanza kuvuta akiwa na darasa la 6, amedai kuwa ili kuipata inawalazimu kwenda nje ya mji kwakuwa wauzaji wakubwa wamekimbia mjini. Msikilize zaidi hapo chini.

MSICHANA ANAYETUHUMIWA KUHUSIKA NA MAUAJI YA KIM JONG-NAM ADAIWA KULIPWA DOLA 90 SAWA TSH 200,000

Mwanamke kutoka Indonesia, aliyekamatwa kwa kuhusika na mauaji ya ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini, anasema alilipwa dola 90 sawa tsh 200,000, kushiriki katika kile alichofikiri, ni kitendo cha mzaha.

Thursday, 23 February 2017

WEMA SEPETU AHAMIA CHADEMA, AUNGANA NA MBOWE MAHAKAMANI.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatarajia kuwakaribisha wanachama wapya waliojiunga leo na chama hicho akiwemo Miss Tanzania wa zamani na muigizaji wa filamu, Wema Sepetu
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilianio wa Chadema, Tumaini Makene amesema leo (Alhamisi) kuwa chama hicho kupitia Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe, baada ya kesi ya kikatiba namba 1 ya mwaka 2017 inayotarajiwa kuwasilishwa Mahakama Kuu leo, kitazungumza kwa umma kupitia .waandishi wa habari kuwakaribisha wanachama wapya waliojiunga leo akiwemo Wema Sepetu.
Wema pamoja mama yake, leo aliongozana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe pamoja na viongozi wengine wa chama hicho kwenye mahakama kuu jijini Dar es Salaam.

Msanii huyo aliyeshinda taji la Miss Tanzania mwaka 2006, alikuwa kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kabla ya kuhamia Chadema.

VIDEO: KUNA COLABLE YA ALLY KIBA NA YVONNE CHAKA CHAKA INAKUJA...

Tizama  simulizi hapo chini kuhusu collabo hiyo ya Yvonne Chakachaka na Alikiba.

Wednesday, 22 February 2017

NASA WATATANGAZA NINI KUHUSU MFUMO WA JUA?

Shirika la Anga za Juu la Marekani (Nasa) leo linatarajiwa kutangaza ugunduzi "mkubwa" kuhusu mambo yaliyomo "nje ya mfumo wetu wa jua".
Hafla ya kutangaza ugunduzi huo itapeperushwa moja kwa moja kupitia runinga ya Nasa na katika mtandao wa shirika hilo mwendo wa saa kumi na mbili jioni (GMT) ambazo ni sawa na saa tatu Afrika Mashariki Jumatano jioni.

JALADA LA MASOGANGE LAKWAMA KWA AG.

Msanii  maarufu anayepamba  video za wasanii wa muziki wa bongo Fleva (Video Queen) Agnes Gerald maarufu Masogange ameendelea kusota rumande, huku jalada lake likiendelea kuwa mikononi mwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

KASHMIR:MARUFUKU MATUMIZI YA ANASA…..

Serikali ya Jimbo la Kashmir nchini India imeweka zuio dhidi ya gharama za anasa.
Wazazi wa bibi harusi watapigwa marufuku kualika zaidi ya wageni mia tano, au mia nne ikiwa mtoto wa kiume atakuwa anaoa.

WABUNGE WAIDHINISHA KILIMO CHA BANGI UHOLANZI.

Bunge la chini nchini Uholanzi, limeidhinisha kuhalalishwa kwa kilimo cha bangi.
Mswada huo ulioidhinishwa utawakinga wakulima wa bangi, ambao wanatimiza masharti fulani dhidi ya kuadhibiwa.

Tuesday, 21 February 2017

WANAWAKE WAPIGWA MARUFUKU KUSAFIRI PEKE YAO LIBYA…

Maafisa wa kijeshi wanaodhibiti eneo la mashariki mwa Libya, wametangaza marufuku kwa wanawake walio chini ya umri wa miaka 60 ya kuwazuia kusafiri nje ya nchi wakiwa peke yao.

MUGABE ASHEREHEKEA KUTIMIZA MIAKA 93…

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, kiongozi wa taifa mwenye umri wa juu zaidi duniani kwa sasa, ametimiza miaka 93.

MZEE AISHI CHINI YA MTI KWA MIAKA 15

Mzee wa miaka 72 ambaye alikuwa Ofisa Elimu Mkoa wa Tanga mwaka 1975, John Kihendo aliyestaafu mwaka 1989, ameamua kuishi chini ya mti kwa muda wa miaka 15 kwa madai kuwa anaitafuta haki ya shamba lake lenye ukubwa wa hekari sita lililoko kata ya Magomeni jijini Tanga.