This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Tuesday, 10 March 2015

LISSU ATANGAZA RASMI ZITTO SI MWANACHADEMA TENA

Mwanasheria mkuu wa chama cha upinzani nchini CHADEMA, Tundu Lissu leo ametangaza kuvuliwa uanachama kwa mbunge wa Kigoma Kasikani Zitto Kabwe baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaamkutupilia mbali pingamizi la mbunge huyo la kuzuia asijadiliwe. "Kwa mujibu wa katiba ya chama cha CHADEMA, mwanachama yoyote anapofungua kesi mahakamani dhidi ya chama chake, endapo atashindwa katika kesi hiyo atakuwa amejiondoa uanachama wake, kwahiyo natangaza rasmi rasmi Zitto Kabwe sio mwanachama tena wa Chadema. Kwa upande wake Zitto Kabwe amesema hawakuwa na wito wa mahakamani leo na Jaji wa kesi kahamishiwa Tabora na hawana taarifa ya Jaji Mpya, pia kaongeza kuwa Mwanasheria anafuatilia na atatoa statement. Licha ya kutupilia mbali kesi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, Mahakama kuu imemtaka kulipa gharama zote za kesi toka ilivyoanza. Mwaka jana Zitto Kabwe aliweka pingamizi mahakamni kuzuia kikao cha Kamati Kuu kumjadili na hoja yake ilikuwa ni kupinga kuitisha kamati kuu kabla shauri lake kusikilizwa na Baraza Kuu

Apple yaja na Saa za kisasa..

Kampuni ya Apple imezindua saa ya kisasa ambayo inauwezo wa kupiga simu,kupokea barua pepe,kucheza muziki na kufuatilia masuala ya afya na mazoezi. Kampuni ya Apple Inc itaanza kuuza saa zake mpya mnamo mwezi April 24 mwaka huu, na bei ya kuanzia sokoni itakuwa dola 10,000 ama paundi 6,611 na bidhaa yake ya kwanza ghali ilitolewa miaka mitano iliyopita katika malengo ya kuongeza wigo wa bidhaa zake hasa vifaa vya simu za mkononi. Sasa hiyo kutoka kampuni ya Apple ya kimichezo kwa zile ndogo zina milimita thelathini na nane itauzwa kwa dola 349 na saa kubwa itauzwa kwa dola 549 na bidhaa ya mwisho itauzwa kwa dola elfu kumi ,hii ni kwa muujibu wa Afisa mtendaji wa kampuni hiyo , Tim Cook said mapema wiki hii.

Mahaka Ivory coast yamhukumu Mke wa Gbagbo miaka 20 gerezani

Mahakama nchini Ivory Coast imemhukumu aliyekuwa mke wa Rais wa nchi hiyo Laurent Gbagbo, kifungo cha miaka 20 gerezani. Simone Gbagbo amehukumiwa kifungo hicho baada ya kukutwa na hatia ya kushiriki katika ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi nchini humo mwaka 2010 na 2011. Simone Gbagbo alikamatwa mwaka 2011 pamoja na mume wake, aliyekuwa rais wa nchi hiyo Laurent Gbagbo, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu katika mahakama ya uhalifu mjini The Hague Uholanzi. Katika ghasia hizo watu takriban elfu tatu walifariki dunia.

Monday, 9 March 2015

Mtoto mwingine Albino akatwa mkono,Waganga wasema vinavyotumika kishirikina..

Matukio ya ukatili dhidi ya albino yanaendelea kuwa tishio nchini,baada ya mtoto wa miaka sita kukatwa kiganja cha mkono Shambulio hilo jipya limetokea mkoani Rukwa kusini magharibi mwa nchi hiyo, ambapo usiku wa kuamkia jana watu wasiojulikana walimshambulia na kumkata kiganja mtoto mwenye umri wa miaka sita, Baraka Cosmas na kisha kutokomea nacho kusikojulikana. Tukio hilo lililotokea katika kijiji cha Kipeta Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga,ambako mtoto huyo anaishi na wazazi wake, Cosmas Yoram (32) na Prisca Shaaban. Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa Jacob Mwaruanda,amesema tukio hilo ni la saa 8 usiku wa kuamkia Jumapili wakati mtoto huyo akiwa amelala na mama yake huku Baba wa mtoto huyo hakuwepo wakati huo. Mkurugenzi wa shirika linalotetea haki za watu wenye ulemavu wa ngozi la Under The Same Sun Vicky Mketema,amezungumzia jinsi ukatili huo unavyofanyika. Na kwanza ameanza kwa kuzungumzia kwa uapnde wa watu ambao wanataka kupata madini,kuwa wanaamini kuwa mguu wa albino unaweza kuwa msaada kwao kufanikiwa katika hilo,msikie hapa chini. https://soundcloud.com/wilberd-kiwale/wanga-wasema-viungo-vya-albino-vinavyotumika

Ngoma ya Odeo ft vocaliser-Ngakukunda Hiii Hapaaa..

Kijana toka mkoani kIlimanjaro anafahamika na wengi kama Odeo hapa nakuwekea link ya kuipata ngoma yake mpya,kamshirikisha kijana mwingine anaekuja vizuri kwenye game anafahamika kama vocaliser. Bofya HAPA https://mkito.com/song/ngakukunda-ft-vocaliser/12897 simu no: +2557565727571

Hii kalii Kondom Zatumika Kama Fasheni za Nywele

Kila kukicha kumekuwa na mambo mapya katika jamii inayotuzunguka na kutokana na utandawazi umetufanya tuone na kujua kila kinachoendelea katika ulimwenguni huu wa sayansi na teknolojia. Kwa sasa kumekuwa na mitindo mbalimbali ya fashion kama kwenye nguo, makeup, viatu na kubwa zaidi kuhusu hii style mpya hapa mjini ya kila mtu kuweka dread kwa namna yake, sasa mama moja wa makamo na raia wa Ghana alitoa mpya baada ya nywele zake kuzivisha kondomu kwa kuzifunga kama dreadlock. Unaionaje hiyo Styl????

Utafiti:Matumizi ya Paracetamol ni hatari kwa Afya..!!!

Matumizi ya kila siku ya dawa za kupunguza maumivu za paracetamol huongeza hatari ya ugonjwa wa moyo,kiharusi na kufupisha maisha ya binadamu, utafiti mpya umeonya. Paracetamol hupendelewa zaidi na madaktari wengi hudai zi salama kulinganisha na aspirin, ambayo imehusishwa na kuvuja damu tumboni na ibuprofen iliyohusishwa na magonjwa ya moyo na kiharusi. Lakini watafiti wa Uingereza waliofanya uchunguzi huo uliowahusisha wagonjwa 666,000 wanasema hatari iliyomo katika dawa hizo,huenda ilipuuzwa na sasa wameagiza uchunguzi ufanywe kuhusu usalama wake. Taarifa hizo iwapo ni za uhakika, itakuwa pigo kwa wengi kwa vile paracetamol zimezoeleka kuliko dawa nyingine yoyote ile ya kupunguza maumivu, na inapatikana kirahisi na kila mahali. Zaidi ya hayo makasha milioni 200 ya paracetamol huuzwa kila mwaka. Hata hivyo Prof. Philip Conaghan wa Taasisi ya Dawa ya Rheumatic and Musculoskeletal mjini Leeds Uingereza, amefichua kuwa matumizi ya muda mrefu ya paracetamol yana athari mbaya kiafya. Professa Conaghan alipitia tafiti nane zilizofanyika huko nyuma, kutathimini uhusiano baina ya matumizi ya muda mrefu ya paracetamol na matatizo ya kiafya kwa watu wazima.
Utafiti huo umebaini wagonjwa wanaopewa dawa hizo za kupunguza maumivu mwilini kwa muda mrefu,wana hatari kubwa ya asilimia 63 kufupisha maisha yao. Hatari ya kupatikana ugonjwa wa moyo na kiharusi iko juu kwa asilimia 68, huku pia kukiwa na hatari kubwa ya asilimia 50 ya kupatikana vidonda vya tumbo au hata kuvuja damu. Watafiti hao walihitimisha kuwa kutokana na ukubwa wa matumizi ya paracetamol na urahisi wa upatikanaji, uchunguzaji wa athari zinazoweza kupatikana kutokana na dawa hizo ulipuuzwa. Una maoni gani juu ya utafiti huu??

Waumini wakatwa sehemu zao za siri ili wamuone mungu!..!!!

Ishu ya imani ni ya mtu binafsi na kila mtu ana uwezo wa kuamini kile anachoona ni sahihi kwa mtazamo wake na mtu anapotokea kumuamini kiongozi wake wa dini kwa asilimia kubwa hutekeleza yale anayofundishwa. Sasa hii ya leo inamuhusu mhubiri maarufu wa dini India ambaye ana wafuasi zaidi ya milioni hamsini duniani Gurmeet Ram Rahim Singh anakabiliwa na mashtaka ya kusababisha majeruhi kwa tuhuma za kuwashawishi wafuasi wake 400 kukata sehemu zao za siri ili waweze kuwa karibu na Mungu.
Wafuasi wa Singh walikata sehemu zao za siri kwenye Hospitali ambayo yeye anaimiliki,ambapo kwenye headlines nyingine mhubiri huyu amekuwa akihusishwa na mauaji ya mwandishi wa habari za uchunguzi pamoja na kutuhumiwa kwa unyanyasaji wa kijinsia lakini hajawahi kushtakiwa. Mmoja wa wafuasi wake Hans Raj Chauhan,aliwaambia Polisi kwamba alikatwa sehemu zake za siri kwa sababu alidhani asingetakiwa kwenye jamii kama angekataa kutekeleza utaratibu huo ulioanzishwa Singh. Singh aliwaambia wafuasi wake kwamba wale ambao wanaotekeleza amri hiyo watakuwa na uwezo wa kumuona Mungu. Vipii wewe unaweza kuwa muumini wa hii dini??

Huyu ni Mbwa anayegundua saratani kwa binaadamu!!

Watafiti wa Marekani wanasema kuwa mbwa amefanikiwa kunusa ugonjwa wa saratani ya koromeo yaani thyroid ambayo wakaguzi walikuwa hawakuiona. Mbwa huyo kutoka Ujerumani kwa jina Frankie alifundishwa kunusa mikojo ya watu walionao na wasiokuwa na ugonjwa huo. Aliweza kugundua saratani ya mgonjwa mara 30 katika visa 34. Wanasayansi wanaona hiyo inaweza kuwa njia mpya ya kukagua saratani hiyo ya koromeo ama thyroid. Wanasema huenda ikayasaidia maeneo tofauti duniani ambayo hayana vifaa vya kuugundua ugonjwa huo. Hiiii imekaa vipi kwa upande wako??

Ndege inayotumia umeme jua yarukwa kwa mara ya kwanza..

Jaribio la kwanza la ndege inayotumia umeme jua limefanyika leo baada ya ndege hiyo kufanikiwa kuanza kuruka asubuhi ya leo juma tatu tarehe 9/3/2015. Ndege hiyo iliruka majira ya saa 12 saa za Afrika Mashiriki ikianzia Abu Dhabi. Ndege hiyo yenye kiti kimoja ina mabawa yenye ukubwa wa jumbo jet huku ndege yenyewe ikiwa na uzito sawa na gari,mabawa yake yamefunikwa na vifaa vya kunasia mionzi ya jua yaani solar panels. Betri zake zina uwezo wa kuhifadhi nguvu ya umeme jua kutoka kwenye jua na hivyo kuiweza kusafiri hata nyakati za usiku. Marubani wawili wanaorusha ndege hiyo Bertrand Piccard na Andre Borschberg watapita katika hatua kumi na mbili za safari yao. Vipi ukipewa deal la kuruka na ndege hiyo nyakati za usiku tuuu ambapo jua halipo??

Saturday, 7 March 2015

WAFANYAKAZI WA RADIO 5 WAPIGWA MSASA NA BBC MEDIA ACTION....

Wafanyakazi wa Radio 5 jijini A rusha wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kitaaluma ili

Wanawake wakulima wanaweza kutokomeza njaa

Wakati wa kuelekea siku ya wanawake duniani,viongozi wa Shirika la Chakula na Kilimo duniani(FAO),Mfuko wa Kimataifa wa Kilimo na Maendeleo(IFAD)na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani(WFP) wamekutana mjini Roma,Italia ili kusisitiza jukumu la wanawake wakulima katika kufanikisha usalama na uhakika wa chakula. Kwa mujibu wa mashirika hayo matatu ya kimataifa,kuwezesha wanawake wakulima na kufikia usawa wa kijinsia kunachangia kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha usalama wa chakula na kupunguza umaskini vijijini. Akizungumza wakati wa mkutano huo mkuu wa IFAD Kanayo Nwanze,amesema nusu ya wakulima sasa ni wanawake wakati ambapo wanaume wanahamia mjini kutafuta riziki. Ameongeza kwamba ni lazima kutambua mchango wa wanawake ambao wanatekeleza kazi ngumu za kuvunja mgongo kwa ajili ya kulisha familia zao. Viongozi hao wamezingatia umuhimu wa kuwapatia wanawake fursa sawa za kufikisha bidhaa zao sokoni,kununua pembejeo na hatimaye kuwa na faida sawa kama wanaume.

Viapo vya ndoa havitekelezeki..!!!

Ahadi ya kuwa pamoja maishani katika shida na raha,taabu na shida viapo hivi ama ahadi hizi zinaonekana kuchukuliwa kirahisi mno na wanandoa wapya, lakini kwa muujibu wa utafiti mpya uliotolewa hivi karibuni unathibitisha kuwa ni rahisi mno kutamka kuliko utekelezaji wa viapo vyenyewe . Mtafiti uliofanywa kwa wanandoa wenye bahati 2,700 waliooana umegundua kwamba ,ikiwa mwanamke katika ndoa hiyo ataugua kwa muda mrefu asilimia sita hukaribia kupewa talaka kuliko wale ambao wana afya njema . Ukilinganaisha na wanaume ambao huugua wakiwa kwenye ndoa,hatari ya kuvunjika kwa ndoa ni ndogo mno,hatahivyo upendo huendelea hadi hapo mmoja wao atakapo baki kuwa mgane ama mjane. Utafiti ulioongozwa na wanazuoni wa chuo kikuu nchini Marekani,kinapendekeza kwamba kwa asili, wanawake wao wameumbwa kutoa huduma katika familia zao na hii inamaanisha kwamba wanaume wao huwa hawana uvumilivu wake zao pindi wanapokumbwa na maradhi ya muda mrefu ,ambayo pia yanweza kuwa hayatabiriki kuyakabili. Walifanyiwa utafiti wanandoa nchini Marekani,ambao wote walikuwa na umri wa miaka 50, mnamo mwaka 1990 ambao waliulizwa juu ya afya zao kuhusiana na maisha yao wakichnugza kwa miaka miwili,miwili ndani ya utafiti uliofanywa kwa miaka ishirini. Asilimia thelathini na mbili ya ndoa ziliishia kwa kuachana na asilimia ishirini na nnenzilivunjika kutokana na vifo vya mmoja wa wanandoa.

Friday, 6 March 2015

Ronaldo huijali mno Sanamu yake

Cristiano Ronaldo mara zote amekuwa na maamuzi ya kipekee yasiyo pitia kwa mtu wa pili na likija suala la kujijali ama kujipenda humwambii kitu hutekeleza ,suala ambalo limemfanya aonekane mchezaji wa kipekee mkubwa na imemjengea heshma kubwa. Lakini mkali huyu wa kabumbu anayesukuma gozi Real Madrid katika kujipenda amepiga hatua moja mbele yenye kuzua mjadala katika mitandao ya jamii na miongoni mwa watu wanaomfahamu ,na kama kinachosema na mtunza makumbusho wa timu Real Madrid ambaye kazi yake kubwa ni utunzaji wa sanamu za wachezaji na kuhakikisha hazipauki na kubaki kama wachezaji halisi walivyo . Gonzalo Presa, ndiye mhifadhi mkuu wa makumbusho hayo ya timu wa Real na ambaye pia ni mkurugenzi wa mawasiliano wa Museo de Cera ,ametema kwamba Ronaldo hutuma kinyozi wake binafsi mara moja kwa mwezi kuhakiki sanamu inayofanana naye iwe na muonekano anaoutaka. Na anasema kwamba Cristiano huwa anataka sanamu hiyo ichanwe nywele mara moja kwa mwezi,na nywele za sanamu hiyo zimeagizwa kutoka nchini India ni nywele halisi . Ronaldo mwenyewe ana makumbusho yake binafsi nchini Ureno,na makumbusho hayo yameendelea kuonesha mambo yamhusuyo tangu mwezi December,mwaka 2013.

Tamko la Facebook lamtia mashakani

Raia mmoja wa Marekani anayefanya kazi katika mataifa ya milki za kiarabu UAE, amekamatwa kwa matamshi aliyochapisha katika mtandao wake wa facebook na sasa anakabiliwa na hukumu ya kufungwa jela. Ryan Pate ambaye ni fundi wa ndege,alikuwa katika likizo ya kujiuguza nyumbani kwake katika jimbo la Florida nchini Marekani wakati alipomkosoa mwajiri wake. Aliita kampuni hiyo kama yenye ''wasaliti na kutoa matamshi ya kibaguzi dhidi ya watu wa mataifa ya milki hiyo. Wakati alipokuwa akirudi alikamatwa kwa kukiuka sheria kali za taifa hilo kuhusu matamshi ya kashfa. Iwapo atapatikana na hatia huenda akahudumia kifungo cha hadi miaka mitano jela.