This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Thursday, 6 July 2017

TCRA YAZITAHADHARISHA KAMPUNI ZA SIMU….

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezitaka kampuni za simu za mikononi nchini, kusitisha matangazo wakati wateja wanapiga simu vinginevyo wataadhibiwa.
Akizungumza jijini hapa leo Alhamisi Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kulaba, amesema kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wateja kuwa wanapopiga simu huanza kusikiliza matangazo ya kampuni hizo badala ya watu wanaowapigia.
Amesema sheria na kanuni za kumlinda mtumiaji wa huduma za mwaka 2011 zinataka watoa huduma kutoa matangazo wakati wa kumjibu mteja anapoulizia salio la muda wa maongezi.
Kulaba amesema watoa huduma wanaweza kutangaza wakati mteja anapopokea taarifa baada ya kuongeza salio na anapoingia katika orodha ya huduma za kampuni husika.
Kulaba amesema wateja wameonyesha hisia ya kukerwa na utitiri wa matangazo yasiyozingatia kanuni za mamlaka hiyo.

Kuhusu adhabu Kilaba amesema kuna aina nyingi za adhabu zinazoweza kutolewa ikiwemo kuzifungia kabisa zisifanye kazi nchini

KUTANA NA MWANAMKE ANAYEFUGA NDEVU….

Harnaam Kaur ni mwanamke anayefuga ndevu,na alilianza kufuga ndevu alipokuwa na umri wa miaka 16.

SIRRO: DAWA YA MOTO NI MOTO………

Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro,amesema wanaotekeleza mauaji dhidi ya raia katika eneo la Kibiti mkoani Pwani wametumwa vibaya, na wao watapelekwa vibaya vibaya.

KABURI LA MTUNZI WA WIMBO WA TAIFA WA UGANDA LAFUKULIWA…

Kaburi la Mtunzi wa Wimbo wa Taifa wa Uganda marehemu George Kakoma limefukuliwa na watu wasio julikana, huku kukiwa na wasiwasi kwamba mabaki ya mwili wake yameibiwa.

UGANDA YAPIGA MARUFUKU WANAWAKE KUVAA SKETI FUPI KAZINI….

Serikali nchini Uganda imewapiga marufuku wanawake wanaofanya kazi katika ofisi za Umma kuvaa nguo fupi na zile zinaoonesha miili yao.

WATU 80 WAFARIKI KATIKA AJALI CAR……

Ajali ya lorry moja la mizigo huko Jamhuri ya Afrika ya kati CAR imesababisha vifo vya zaidi ya watu 80, wengi wakiwa wachuuzi waliokuwa wakielekea sokoni mjini Bambari.

RAIS WA ZAMBIA ATANGAZA HALI YA DHARURA...

Rais wa Zambia Edgar Lungu ametangaza hali ya dharura nchini humo kutokana na moto mkubwa uliyotekteza soko kuu la mjini Lusaka.

MAREKANI: TUTATUMIA NGUVU ZA KIJESHI DHIDI YA KOREA KASKAZINI...

Marekani imesema kuwa itatumia nguvu za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini ''iwapo ni lazima'' kufuatia jaribio la kombora la masafa marefu lilotekelezwa na taifa hilo.

Monday, 3 July 2017

FAO: IDADI YA WATU WALIOATHIRIWA NA NJAA ITAONGEZEKA…

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limesema kuwa, watu milioni 20 wanasumbuliwa na njaa na utapiamlo lote duniani.

UFARANSA YACHANGIA EURO 250,000 KUSAIDIA WAKIMBIZI TANZANIA……

Msaada wa fedha kwa wakimbizi unawawezesha kujikwamua kiuchumi
Serikali ya Ufaransa imechangia kiasi cha Euro 250,000 kwa shirika la mpango wa chakula duniani, WFP ili wakimbizi nchini Tanzania waweze kupata msaada zaidi wa kifedha.

RUGEMARILA NA BOSI WA IPTL WAONGEZEWA MASHTAKA 6….

Mkurugenzi wa kampuni ya VIP Engeneering na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL, James Rugemalira (kushoto) na Habinder Seth Sigh (kulia) Mwenyekiti Mtendaji wa PAP.

SAMSUNG YATUMIA SEHEMU ZA NOTE 7 KUUNDA SIMU MPYA…..

Kampuni ya mawasiliano ya Samsung imeanza kuuza simu nyingine ambazo inasema imetumia baadhi ya sehemu na vipande vilivyokuwa kwenye simu za Galaxy Note 7 ambazo zilikumbwa na matatizo.

Friday, 30 June 2017

VIDEO:WIZARA MAMBO YA NDANI, IGP SIRRO WANAZUNGUMZA KUHUSU MAUAJI KIBITI


Thursday, 29 June 2017

CCM WANAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI

June 29, 2017 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi ‘CCM’ Humphrey Polepole anaongea na Waandishia wa Habari Ofisi ndogo ya CCM Lumumba DSM.

UTAFITI:BODABODA HUWANYANYASA WASICHANA KIMAPENZI….

Wafanyabiashara ya huduma za usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda, wametajwa katika utafiti kuwa wanaowanyanyasa kimapenzi na kuwafanyia ukatili wasichana wanaokataa kushirikiana nao kimapenzi.