This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Tuesday, 6 March 2018

WAANDAMANA KUOMBA RAIS ADHIBITI ULEVI WA WANAUME….

Mamia ya wanawake katika vijiji vya Kirangi na Kuri Kiambu nchini Kenya, wameandamana Jumapili iliyopita wakipinga ongezeko la vilabu vya pombe (bars) na ulevi wa waume zao.

WACHUNGAJI 6 WA MAKANISA YALIYOFUNGWA RWANDA WAKAMATWA..

Polisi nchini Rwanda imetangaza kuwatia kizuizini wachungaji 6 na viongozi wa makanisa, kutoka baadhi ya makanisa yaliyofungwa kwa amri ya serikali ya nchi hiyo.

AOMBA KUPELEKWA KWA MGANGA BADALA YA JELA…….

Mwanaume mmoja kwa jina la Wilson Obeka anaekabiliwa na mashtaka ya jinai, aliwashangaza wengi mahakamani huko Eldoret baada ya kumuomba hakimu apelekwe kumuona mchungaji au mganga badala ya kwenda jela.

VIDEO: MOTO WATEKETEZA SOKO LA MBAGALA….

Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu–Dar, asubuhi ya leo Machi 6, 2018.

Monday, 5 March 2018

INSPEKTA WA POLISI NA WAZIRI WA ULINZI WAFUKUZWA KAZI…

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amemfuta kazi Inspekta mkuu wa polisi Kale Kayihura na waziri wa Ulinzi Henry Tumukunde.

Sunday, 4 March 2018

WATU WAPIGA KURA UCHAGUZI MKUU ITALIA…

Watu nchini Italia wanapiga kura baada ya kampeni zilizoangazia zaidi masuala la uhamiaji na uchumi.

TMA YATOA TAHADHARI KWA WANANCHI…….

Mamlaka ya hali ya hewa iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania imewatahadharisha wananchi kuwepo kwa hali mbaya ya hewa katika maeneo yote ya pwani kuanzia leo usiku.

MWANAFUNZI MTANZANIA AUAWA KIKATILI AFRIKA KUSINI………….

Mwanafunzi wa Tanzania aliyekuwa akisoma nchini Afrika Kusini,Baraka Nafari aliyekuwa akichukua Shahada ya Uzamivu (PHD) katika Chuo Kikuu cha Johannesburg (UJ) ameuawa kikatili Ijumaa Februari 23, mwaka huu kwa kugongwa na gari mara mbili na kubamizwa kwenye ukuta na baadaye kushambuliwa kwa visu.

MWANAMUME AJIPIGA RISASI NA KUJIUA NJE YA WHITE HOUSE….

Mwanamume mmoja amejipiga risasi na kujiua nje ya Ikulu ya Marekani ya White House mjini Washington, kikosi cha kumlinda rais kimesema.

Tuesday, 27 February 2018

BABA MKWE AMLAZIMISHA MKE WA MWANAE KUMPIGA BUSU…!!

Maajabu kweli mengi yanatokea hasa tukifanya vitu kupitiliza nikimaanisha nini, kuna bwana mmoja kutoka Yancheng China alilewa kupitiliza jambo lililopelekea kumpiga busu kwa lazima mke wa mwanae siku ya harusi yao.
Tukio hilo liliwaudhi watu wengi hasa wanafamilia wa pande zote mbili na kuzua ugomvi baina yao.
Wanandoa hao wameumizwa na kitendo hicho sana, ukizingatia video ya tukio hilo imezidi kusambaa katika mitandao ya kijamii.
Police wamedai kuwa wamefanya uchunguzi na tukio hilo lilitokea 22 mwezi wa pili.
Familia imeomba watu waache kuisambaza video hiyo kwani haileti picha nzuri kwa jamii.

HUU NI UTAMADUNI WA AJABU NAMIBIA…..

Katika nchi ya Namibia kuna mambo mengi mazuri ya kuifanya nchi hiyo itembelewe na watu mbali mbali hasa kwenye swala la kuenzi na kuziendeleza tamaduni zao.

NYOKA MWENYE SUMU KALI AGUNDULIWA NDANI YA MKEBE WA CHAKULA CHA MTOTO AUSTRALIA……….

Mwanamke amegundua nyoka mwenye sumu kali ndani ya mkebe ambao mtoto wake anatumia kebeba chakula cha mchana nchini Australia.

WAKUU WA MAJESHI WAFUTWA SAUDI ARABIA………..

Saudi Arabia imewafuata makamanda wa vyeo vya juu jeshini, akiwemo mkuu wa majeshi.
Mfalme Salman pia amefanya mabadiliko kwa makanda wa vikosi vya nchi kavu na vile vya angani.

RAMAPHOSA ATANGAZA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI…

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, ametangaza baraza lake jipya la mawaziri.
Waziri wa zamani wa fedha Nhlanhla Nene amerejeshwa tena katika nafasi hiyo.

Monday, 26 February 2018

SUGU, MASONGA WAHUKUMIWA JELA MIEZI MITANO.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya imewatia hatiani mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Emmanuel Masonga, na kuwahukumu kifungo cha miezi mitano jela.