Watu 31
wamenusurika kifo baada a ndege ya Etihad EY 474 waliyokuwa wakisafiria kutoka
Abu
Dhabi kuelekea Jakarta kupata hitilafu ikiwa angani.
Msemaji wa shirika hilo aliliambia Shirika la Habari la AFP kwamba,
abiria tisa kati ya hao walijeruhiwa na kulazwa hospitalini nchini Indonesia.
Alisema ajali hiyo ilitokea muda mfupi baada ya ndege hiyo kuruka
ikitokea Indonesia.Hali hiyo ilisababisha tafrani kwa abiria ambao baadhi yao
walipata majeraha kutokana na mshtuko.
Alisema wataalamu wa shirika hilo walikwenda Indonesia kwa ajili ya
uchunguzi wa ndege hiyo ili kubaini tatizo.
Vilevile walikutana na wanafamilia kadhaa wa majeruhi na
kuthibitisha kuwa shirika lao litagharimia matibabu.
Rais wa Shirika la Ndege la Etihad na Mkurugenzi Mkuu James Hogan
alisema: “Rubani wetu na wafanyakazi wa ndege wanapaswa kupongezwa kwa utulivu
wao na namna ambavyo walivyoshughulikia tukio hilo na huduma waliyoionyesha kwa
abiria japo kuwa abiria wachache walijeruhiwa,’’ alisema na kuiongeza: “Ni
ushahidi wa mafunzo ya kiwango cha juu yanayotolewa kwa wafanyakazi wetu,”
alisema.
0 comments:
Post a Comment