Thursday, 5 May 2016

HALI YA HATARI YATANGAZWA CANADA….

Gavana wa jimbo la Alberta nchini Canada, ametangaza hali ya hatari wakati moto mkubwa wa
msituni unapoteketeza maeneo ya mji wa Fort McMurray.
Maafisa wanasema kuwa nyumba elfu 1 mia 6 na majengo mengine yameharibiwa na moto huo, ambao sasa unakaribia uwanja wa ndege wa mji huo.
Waziri mkuu nchini Canada amesema kuwa,moto huo umesababisha hasara ya kiwango kikubwa.

Watu wa mji wa Fort McMurray ambao wanafikia elfu  80 wamehamiswa kutoka eneo hilo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment