Mwanamke mmoja nchini India amejifungua mtoto wa uzani wa kilo 6.8,
ambaye madaktari
wanasema huenda akawa mtoto mwenye uzani wa juu zaidi kuwahi
kuzaliwa nchini humo.
Mtoto huyo ana uzani sawa na mtoto wa umri wa miezi
sita.
Nchini humo watoto wengi huzaliwa na uzani wa kadiri
wa kilo 2.5 mpaka 3.5.
Mamake Nandini 20 alijifungua kupitia upasuaji katika
jimbo la Karnataka, kusini mwa nchi hiyo.
Visa vya watoto kuzaliwa na uzani wa juu kupindukia
sana, hutokana na mama kuugua kisukari lakini madaktari wamebaini Nandini hana
tatizo hilo.
Rekodi ya mtoto mwenye uzani wa juu zaidi India
inashikiliwa na mvulana aliyezaliwa na Firdous Khatun jimbo la Uttar Pradesh
Novemba 2015.
Mvulana huyo alikuwa na uzani wa kilo 6.7.
Rekodi ya dunia inashikiliwa na mvulana aiyezaliwa na Carmelina
Fedele eneo la Aversa Italia, mwezi Septemba 1955 ambaye alikuwa na uzani wa
kilo 10.2.
0 comments:
Post a Comment