Mji
mmoja nchini Uzbekistan umekua ukiwapa waalimu wake kuku kama mshahara badala
ya pesa.
Mamlaka
za mji wa Nukus katika jimbo linalojitawala la Karakalpakstan, wamekua wakitoa
vifaranga wachanga kwa walimu kutokana na uhaba wa pesa nchini humo.
Kituo cha radio kinachofadhiliwa
na Marekani Radio Ozodlik, kimemnukuu mwalimu mmoja akilaani hatua hiyo kama
aibu kubwa kwa mamlaka.
Mwalimu huyo aliyeghadhabishwa na
hatua hiyo amesema kuwa,hataki vifaranga kwa sababu anaweza kuwapata sokoni
lakini wanataka pesa zao.
Vifaranga wanaotolewa kama
mshahara wana gharama ya dola mbili kila mmoja, ikiwa ni maradufu bei inayouzwa
vifaranga sokoni.
Mamlaka za Uzbekistan hazikubalii
uhuru wa vyombo vya habari, na raia wa huko hutegemea vyombo vya habari vya
kimataifa kutoa sauti yao, ila hawajitambulishi.
Uzbekistan imekumbwa na uhaba wa
fedha kwa miaka kadhaa sasa, hali inayosababisha serikali kuchelewesha
mishahara ya wafanyikazi na malipo ya uzeeni.
Mapema mwezi huu wafanyikazi wa
serikali katika mji mkuuTashkent, walilalamikia kwamba hawakuwa wamelipwa
mshahara kwa miezi miwili kwa sababu benki hazikuwa na pesa.
0 comments:
Post a Comment