Mwanamke
mmoja kati ya wanne waja wazito hutoa mimba kila mwaka, takwimu kutoka shirika
la
afya duniani na taasisi ya Gutt macher zinaashiria.
Ripoti hiyo kutoka jarida la Lancet
inasema kuwa, visa milioni 56 vya utoaji mimba hufanyika kila mwaka, kiwango
kilicho juu kuliko ilivyodhaniwa.
Watafiti wanakiri kuwa viwango hivyo
vimeimarika katika nchi nyingi tajiri, lakini wanaonya kuwa linaficha ukosefu
wa mabadiliko katika maeneo maskini katika miaka 15 iliopita.
Wanasayansi wanasema idadi ya visa
vya utoaji mimba kila mwaka, vimeongezeka kutoka milioni 50 kwa mwaka kati ya
mwaka 1990-1994 hadi milioni 56 kwa mwaka kati ya 2010-2014.
Ongezeko hilo linashuhudiwa zaidi
katika nchi zinazoendelea, chanzo kikuu kikiwa ni ongezeko la idadi ya watu na
haja ya kuwa na familia ndogo.
Hesabu inaonyesha kwamba wakati visa
vya utoaji mimba vinasalia kama vilivyo katika mataifa maskini, katika maeneo
tajiri visa hivyo vimeshuka kutoka wanawake 25 hadi 14 kati ya wanawake 100
walio katika umri wa kuzaa.
Amerika kusini imetajwa kuwa kati ya
wanawake 3 mmoja hutoa mimba, kiwango kilicho juu kuliko eneo lingine duniani.
0 comments:
Post a Comment