Bunge la Seneti Brazil limepiga kura kuamua kuidhinisha
kura ya kutokuwa na imani dhidi ya kiongozi wa taifa hilo Dilma Rousseff.
Atasimamishwa kazi ya urais kwa
siku zisizozidi 180 wakati bunge hilo la Seneti litakagua tuhuma zinazomkabili.
Bi Rousseff anatuhumiwa kubadili
kinyume cha sheria fedha za serikali kuficha nakisi inayoongezeka ya umma
kufuatia kuchaguliwa kwake tena mnamo 2014, tuhuma anazozikana.
Masenata 55 waliunga kuidhinishwa
kura hiyo ya kutokuwana imani dhidi ya 22 bungeni katika kikao cha zaidi ya saa
20.
Makamu wa rais Michel Temer sasa
ndio atashikilia madaraka wakati kesi dhidi ya Bi Rousseff inaendelea.
Rousseff alichukua hatua ya
mwisho kujiokoa kwa kukataa rufaa katika mahakama ya juu zaidi nchini humo
kusitisha kura hiyo, lakini hatua hiyo ilipingwa.
0 comments:
Post a Comment