Mapambano
kati ya vyombo vya dola na wafanyabiashara wanaodaiwa kuficha sukari
yameendelea
maeneo mbalimbali nchini huku mifuko ya bidhaa hiyo
ikikamatwa mkoani Mwanza.
Taarifa kutoka mkoani Mwanza zinasema Kikosi cha Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo, kimekamata mifuko 800 kati ya 1,200 ya
kilo 50 ambayo ilikuwa ikishushwa kwenye ghala la mfanyabiashara
mmoja kwa ajili ya kufichwa.
Sukari hiyo ilikamatwa juzi jioni katika Mtaa wa
Rufiji, Mwanza ikiwa kwenye gari ya Scania namba
T 200 BSV na tela lake namba T
601 DFM, ikiwa limeegesha katika ghala la Adam Michael Balenga.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Augustine Senga alisema
baada ya kukamatwa sukari hiyo mhusika alidai ilikuwa imetoka
Kampuni ya Al Naem Enterprise Ltd ya Tabata, Dar es Dar es Salaam.
“Tumekamata sukari mifuko 800 ya kilo 50. Hii ilikuwa ikiuzwa
kwa siri nyumbani kwa mfanyabiashara, wakati tunakamata tayari kiasi kingine
cha mifuko 400 ilikuwa imekwisha kuuzwa,” alisema Senga.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema kikosi kazi
kimeanza kazi vizuri na bado kinafuatilia nyendo za baadhi ya
wafanyabiashara ambao wanaonekana kuanza kutoa sukari na kuiuza kwa siri baada
ya agizo la Rais Dk. John Magufuli.
0 comments:
Post a Comment