Tuesday, 3 May 2016

UANDISHI WA HABARI KAZI HATARI DUNIANI..!!

Kazi ya uandishi wa habari inaendelea kuonekana ni ya hatari zaidi duniani, baada ya utafiti
uliofanyika mwaka jana pekee, kubaini jumla ya waandishi mia 1 na 10 waliuawa.

Utafiti wa mwaka jana umebainisha kuwa kati ya wanahabari hao waliouwa, 71 wameuawa wakitekeleza majukumu yao ya kikazi.
Hayo yameelezwa leo na Mwenyekiti wa Misa Tanzania Simon Berege jijini Mwanza, katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani, ambayo huadhimishwa Mei 3 kila mwaka.

Kwa mujibu wa Berege hakuna kifo kilichotokea Tanzania, bali kulitokea kesi 30 za unyanyasaji wa wandishi wa habari kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu, gazeti moja kufutwa, vituo kadhaa vya redio kufutiwa leseni huku mwanahabari akijeruhiwa akiwa kazini baada ya kuvunjwa mguu.

0 comments:

Post a Comment