Karani
mmoja wa kupokea wageni mjini London, alilazimika kurudi nyumbani baada ya
kukataa
kuvaa viatu vyenye visigino virefu (High hills) imebainika.
Mfanyakazi huyo wa kampuni
ya Temp Nicola Thorp mwenye umri wa miaka 27 kutoka Hackney, amewasili katika
kampuni moja inayoshughulikia maswala ya kifedha PwC, kabla ya kuarifiwa kwamba
anahitajika kuvaa viatu vyenye visigino vya nchi 2 hadi 4.
Alipokataa na kulalamika
kwamba mbona wenzake wa kiume hawakutakiwa kuvaa hivyo, alitakiwa kurudi bila
ya mshahara.
Kampuni ya Portico imesema
kuwa iliweka sheria hizo kwa wafanyikazi wanaokabidhiwa PwC, na imesema kuwa
haitaondoa sheria hiyo.
0 comments:
Post a Comment