Wizara ya Habari, utamaduni, sanaa na michezo imefungia video na
wimbo wa "chura" ulioimbwa na msanii Snura Mushi.
Msanii huyo pia amefungiwa kufanya
maonyesho ya wazi kwa sababu imebainika kwamba hana kibali kutoka Basata
kinachomtambua kama msanii.
Msemaji wa wizara hiyo, Zawadi Msalla
amesema wizara ilikaa na Basata, TCRA, bodi ya filamu na Snura mwenyewe na
kufikia uamuzi wa kuufungia wimbo huo kwa sababu unadhalilisha, hauna maadili
na unakiuka haki za binadamu.
Msalla amesema wizara imemtaka msanii
huyo kuutoa wimbo huo kwenye mtandao wa YouTube na chombo chochote hakitakiwi
kupiga wimbo wala kuonyesha video hiyo.
"Mtu yoyote atakayeendelea
kusambaza wimbo au video ya chura atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria ya
makosa ya mtandao. Kwa hiyo wananchi wajihadhari katika hilo," amesema Msalla.
0 comments:
Post a Comment