Shirika la Kimataifa
la Polisi linawasaka raia wawili wa Scotland, wanaodaiwa kukimbilia Tanzania
baada ya kufanya udanganyifu na kujipatia Paundi 20 milioni za Uingereza (sawa
na Sh62 bilioni).
Wawili hao Gareth
Johnson (48) na Geoffrey Johnson (72) walikuwa sehemu ya kundi la watu 18,
lililohusishwa na uhalifu huo wa uchakachuaji ongezeko la kodi ya simu za
mkononi nchini Uingereza.
Kutokana na kosa
hilo Mahakama Maalumu ya Mapato na Forodha ya Uingereza (HMRC), iliamuru
wanafamilia hao ambao ni baba na mwanae, walipe fidia ya Paundi 109 milioni
(sawa na Sh337 bilioni).
Lakini hukumu hiyo
ilitoka bila ya wawili hao kuwapo baada ya kutoroka kabla ya shauri hilo kuanza
kusikilizwa na inasemekana walikimbilia Tanzania.
Akizumgumzia suala
hilo Mkuu wa Interpol Tanzania Gustavus Babile, amesema kibali cha kimataifa
cha kukamatwa kwa wawili hao kipo kwenye tovuti yao.
Amesema walipokea
taarifa kutoka Uingereza hivyo hatua inayofuata ni kukipeleka kibali hicho
mahakamani kwa ajili kupata nguvu za kisheria za nchi.
Hadi sasa inadaiwa
kuwa Geoffrey na kijana wake wamekuwa mafichoni Tanzania kwa takriban miaka
mitatu sasa.
0 comments:
Post a Comment