Friday, 6 May 2016

WAHUDUMU WA AFYA WATAKIWA KUNAWA MIKONO ILI KUPUNGUZA MAAMBUKIZI KWA WAGONJWA..!!

Shirika la afya duniani limewataka wahudumu wa afya kuimarisha usalama wa wagonjwa, kwa kuzingatia misingi ya usafi wa mikono ili kupunguza idadi ya maambukizi.


WHO imetoa wito huo jana katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kunawa mikono, inayoadhimishwa kila mwaka Mei 5.

Shirika hilo linasema maambukizi mengi hutokea wakati vijidudu vinapotoka kwenye mikono ya wahudumu wa afya, kwenda kwa wagonjwa.



WHO inasema usafi wa mikono unaweza kuokoa maisha ya watu milioni 8 kote duniani, na imetoa wito wa vituo vya afya kujiunga na kampeni ya "Okoa maisha, nawa mikono.

0 comments:

Post a Comment