Thursday, 5 May 2016

ALIYEJARIBU KUUZA MWANAWE AHUKUMIWA MIAKA 5…!!

Mahakama moja nchini Afrika kusini imemhukumu mwanamke mmoja kifungo cha miaka 5, kwa
kujaribu kumuuza mwanawe kupitia mtandao wa kuuza na kununua wa Gumtree.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 20 atatumikia kifungo chake akiwa nyumbani, kwa sababu mahakama hiyo iliona kheri impe fursa ya kumlea mwanawe.
Msemaji wa mamlaka ya mashtaka ya umma Natasha Kara, anasema manamke huyo alinaswa na mtego wa afisi yao baada ya afisa mmoja kujidai kuwa ni mteja.
Akijitetea mwanamke huyo aliiomba mahakama imhurumie, kwani alizongwa na mawazo na ufukara baada ya mumewe kususia kumsaidia kumlea alipogundua kuwa hakuwa wake.

Hapo ndipo akaamua kumpeana ila alikosa njia mwafaka, na akalazimika kutumia mtandao huo wa kuuza Gumtree.

Related Posts:

  • WAKATI BORA WA KUPEWA CHANJO YA HOMA… Na utafiti nchini Uingereza unaonesha kuwa, chanjo ya homa ni bora zaidi iwapo mtu atapewa majira ya asubuhi badala ya alasiri. Watafiti wamebaini kuwa uwezo wa mwili wa mtu una nguvu mno kuwa na matoke bora iwapo mtu a… Read More
  • MAELFU WAANDAMANA NORTH CAROLINA…. Maelfu ya waandamanaji wamesafirishwa kwa mabasi hadi katika mji mkuu wa jimbo la North Carolina nchini Marekani ili kufanya maandamano. Waandamanaji hao wameenda ili kuunga mkono na wengine kupinga sheria mpya ya kit… Read More
  • UKILALA KATIKA KITANDA KIPYA HUTALALA VYEMA…!! Je ushawahi kugundua kuwa ukilala katika kitanda au mazingira mapya haupati usingizi wa kutosha? Sasa Utafiti umebaini kuwa mtu akilala katika mazingira mapya ubongo wake haulali wote! Upande wa kushoto wa ubongo huw… Read More
  • MKE WA KIBAKI AFARIKI…… Mke wa Rais mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki Lucy Kibaki, amefariki dunia leo jijini London, Uingereza alipokuwa akipatiwa matibabu. Kwa mujibu wa taarifa ya Rais Uhuru Kenyatta, Lucy Kibaki amefariki katika hospitali ya … Read More
  • KICHAA CHA MBWA HUU WATU ZAIDI YA 1000 KILA MWAKA NCHINI…. Imeelezwa kuwa watu elfu 1 mia 6 hasa watoto hufa nchini kila mwaka, kutokana na ugonjwa wa kichaa cha mbwa. Hayo yalielezwa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Mary Mashingo. Dk Mashingo … Read More

0 comments:

Post a Comment