Monday 2 May 2016

TANZANIA NI NCHI YA PILI AFRIKA, AMBAYO UCHUMI WAKE UNAKUA KWA KASI…..

Shirika la fedha duniani IMF, limeitaja Tanzania kama nchi ya pili Afrika ambayo uchumi wake unakua kwa kasi.

IMF imesema kwa ukuaji wa asilimia 6.9, Tanzania ipo chini ya Ivory Coast yenye asimilia 8.5.
Wamesema Tanzania itaendelea kufanya vizuri kutokana na kuongezeka kwa uwekezaji, hasa kwenye mafuta, gesi pamoja na maboresho ya miundombinu, na kuifanya kuwa sehemu muhimu ya usafirishaji Afrika.

Hii ni orodha rasmi ya nchi za Africa, ambazo uchumi wake unakua kwa kasi.


1 Ivoire Coast 8.5%
2 Tanzania 6.9%
3 Senegal 6.6%
4 Djibouti 6.5%
5 Rwanda 6.3%
6 Kenya 6.0%
7 Mozambique 6.0%
8 Central African Republic 5.7%
9 Sierra Leone 5.3%
10 Uganda 5.3%

0 comments:

Post a Comment