Madaktari
nchini Uingereza wamefanikiwa kwa mara ya kwanza kupandikiza viungo vya watu
wanaougua Ukimwi kwenye wagonjwa wanaougua Ukimwi.
Kwa jumla, figo mbili na maini
mawili vilipandikizwa kwa watu waliokuwa wameathirika sana na Ukimwi.
Viungo vilitolewa kwa watu baada
yao kufariki.
Wataaamu wanasema mafanikio hayo
yatasaidia kupunguza uhaba wa watu wanaoweza kutoa viungo na wanatumai kwamba
watu zaidi wanaougua Ukimwi watajitokeza kutoa viungo vyao.
Kwa jumla, nchini Uingereza, watu
watatu hufariki kila siku wakisubiri kupata viungo vya kupandikiziwa.
Ingawa kwa sasa viungo vya watu
wenye Ukimwi vinaweza tu kutolewa kwa watu wanaougua Ukimwi, mtaalamu wa
upandikizaji Prof John Forsythe anasema hilo bado litasaidia kwa sababu
litawezesha kufanyika kwa upandikizaji katika hali ambazo awali haingewezekana.
Upandikizaji wa kwanza wa figo
kwa watu wanaougua Ukimwi ulifanyika katika hospitali za Guy na St Thomas'
Hospital jijini London mwaka 2015.
0 comments:
Post a Comment