Jaji
mmoja mzungu nchini Afrika Kusini ameshutumiwa vikali, baada ya kudaiwa kusema
kwenye mitandao ya kijamii kwamba ubakaji ni kawaida kwa wanaume weusi.
Jaji Mabel Jansen alisema unajisi
wa watoto na wasichana na pia ubakaji wa wanawake, ni jambo la kufurahiwa la
kupitisha miongoni mwa Waafrika.
Kadhalika amenukuliwa pia akisema
hajawahi kukutana na msichana mweusi ambaye hajawahi kubakwa.
Akijitetea jaji huyo amesema
amefasiriwa vibaya na kwamba matamshi hayo yametumiwa vibaya nje ya muktadha.
Jaji Jansen anadaiwa kutoa
matamshi hayo kwenye mawasiliano na mwanaharakati Gillian Schutte kwenye
Facebook mwaka jana lakini yamesambazwa sana wikendi.
Wakili mashuhuri Afrika Kusini
Vuyani Ngalwana amesema kuwa, matamshi hayo ya jaji huyo yanawaharibia sifa
wanaume wote weusi na kuwaonesha kama wabakaji.
Amesema ni maneo ya kushangaza
sana kwa mujibu wa gazeti la Business Day.
Kampeni
imeanzishwa nchini humo ya kutaka jaji huyo afutwe kazi.
Bw Ngalwana amesema Tume ya Huduma za Mahakama inafaa
kumtaka afafanue matamshi hayo kabla ya kumchukulia hatua.
Msemaji wa chama tawala cha
African National Congress (ANC), amesema anashuku kuna majaji wengi wenye
mtazamo wa kibaguzi.
Utawala wa Wazungu ambao
ulihalalisha ubaguzi wa rangi, ulifikia kikomo nchini Afrika Kusini mwaka 1994.
0 comments:
Post a Comment