Tuesday, 10 May 2016

SERIKALI KUU MAREKANI YAISHTAKI NORTH CAROLINA….!!

Idara ya sheria nchini Marekani, imeifungulia mashtaka serikali ya jimbo la North Carolina
pamoja na gavana wake, ili kuzuia utekelezwaji wa sheria mpya kuhusu jinsia.

Sheria hiyo inawalazimisha watu waliobadili jinsia kutumia vyoo vinavyokwenda sambamba na jinsia waliyotambuliwa nayo wakati wa kuzaliwa.

Mkuu wa sheria Loretta Lynch, amesema anatafakari kusitisha msaada unaotolewa na serikali kuu, kufadhili taasisi za serikali ya jimbo la North Carolina.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment