Wanasayansi wanadai kuunda aina ya ngozi inayoweza kubandikwa juu ya
mwili wa mtu kupunguza muonekano wa mikunjo ya ngozi mwilini na ngozi
inayopwaya chini ya macho kutokana na uzee.
Ni aina ya maji maji
mtu anayopaka mwilini alafu inaachwa kukauka ambapo baadaye husihia kuwa ngozi
nyembamba iliyo mithili ya 'ngozi ya ujana, Nature Materials inaarifu baada ya
kufanya majiribio kadhaa madogo.
Kwa sasa inafanyiwa
majaribio ya kuuzwa kama bidhaa ya urembo.
Lakini wanasayansi
Marekani wanasema "ngozi ya pili " huenda baadaye ikaweza kutumika
kutengeneza dawa na kinga dhdi ya jua.
Ngozi ya pili
Kundi la wanasayansi
kutoka chuo kikuu cha Havard kitengo cha matibabu na taasisi ya teknolojia Massachusetts
wamefanya majaribio ya bidhaa hiyo kwa watu waliojitolea ambao walipakwa ngozi
hiyo chini ya macho, kwenye mikoni yao na miguu.
Ngozi hiyo inayotokana
na kemikali polysiloxane polymer iliundwa kwenye maabara kwa kutumia chembe
chembe za Silicone na hewa safi ya Oxygen.
Licha ya kwamba sio
ngozi ya kweli lakini imeundwa kuiga ngozi asili na pia kuacha nafasi ya hewa
kupita.
Kwa mujibu wa
watatfiti ngozi hiyo bandia ina uwezo wa kunasa mvuke na kusaidia ngozi
kujivuta kiasi cha inavyostahili.
Wakati ngozi ikizeeka inanyauka na kwa
hivyo haitoi matokeo mazuri vile kwenye majaribio haya.
Watafiti
wanasema ngozi hiyo bandia haionekani na inaweza kubandikwa kwa siku nzima bila
kuwa na madhara yoyote na inaweza kuhimili vitu kama jasho na mvua.
Lakini utafitia
zaidi unahitajika. Ni lazima pia wakaguzi watoe idhini kwamba ni salama
kutumiwa.
Dr Tamara
Griffiths wa muungano wa madaktari wa ngozi Uingereza anasema ngozi ya chini ya
macho hupwaya au kufura kutokana na mkusanyiko wa mafuta katika sehemu hiyo inayohusishwa
na uzee.
Licha ya kwamba
ni hali ya kawaida lakini watu wengi hujaribu mbinu tofuati kuziondoa, wengine
hata kufanyiwa upasuaji.
Dr Griffiths
amesema: "matokeo ya ngozi ya polymer yanayonyesha kuwa sawana kufanyiwa
upasuaji bila ya hatari za upasuaji . Utafiti zaidi unahitajika, lakini huu ni
mtazamo mzuri ulio na matumaini makubwa kwa tatizo la wengi. Nitafuatilia
maendeleo ya utafiti huu kwa makini."
0 comments:
Post a Comment