Tuesday, 3 May 2016

WHATSAPP YAFUNGWA KWA SAA 72 BRAZIL..!

Hakimu mmoja nchini Brazili amefunga mawasiliano ya mtandano wa simu kwa njia ya whatsapp kwa saa 72.

Hakimu huyo Marcel Montalvao amesema kampuni inayomiliki mtandao huo imeshindwa kusaidia kutoa taarifa katika kesi ya uhalifu.
Mwezi Machi Montalvao aliamuru kukamatwa kwa afisa mwandamizi wa Facebook katika nchi za Kilatini bwana Diego Dzoran, baada ya kukataa kutoa ushirikiano katika uchunguzi dhidi ya dawa za kulevya.
Whatsapp mtandao unaomilikiwa na Facebook umesema umekatishwa tamaa na kitendo hicho, kwa kuwa wamekuwa wakitoa ushirikiano wa kutosha mahakamani.

Mtandao huo umekuwa ukifungiwa mara kadhaa nchini Brazil kwa miezi michache ya karibuni kwa sababu zinazofanana na hizo.

Related Posts:

  • Mexico yahalalisha bangi kwa watu 4 tu….. Jana nilikuwa na story inayohusu bangi, ambapo wapiga kura katika jimbo la Ohio nchini Marekani, wamekataa pendekezo la kuhalalisha matumizi ya bangi katika jimbo hilo. Sasa leo nakupitishia story inayofanana na hivyo … Read More
  • Video: Hii single inaweza kukufariji sanaa Ni single ya Goodluck Gozbert, mwimbaji ambaye pia ni Producer wa mziki na skillz zake zimehusika kuzisuka nyimbo kadhaa za Mo Music ikiwemo ‘basi nenda‘ … Read More
  • Usikose kusoma nakala ya gazeti la TABIBU kesho alhamisi                                               &n… Read More
  • Wachina kusubiri hadi Machi kupata watoto wawili……….. Mamlaka kuu inayosimamia upangaji wa uzazi nchini Uchina, imeonya wanandoa nchini humo kwamba sharti waendelee kutii agizo la kuwa na mtoto mmoja kwenye familia hadi sheria ifanyiwe marekebisho mwezi Machi. Alhamisi ya… Read More
  • Wapiga kura wakataa kuhalalisha bangi Ohio....!! Wapiga kura katika jimbo la Ohio nchini Marekani, wamekataa pendekezo la kuhalalisha matumizi ya bangi katika jimbo hilo. Pendekezo hilo lililopewa jina Issue 3, lingefanyia marekebisho sheria ya jimbo la Ohio na kuifany… Read More

0 comments:

Post a Comment