Mwongoza
Watalii (Guide), ambaye anadaiwa kupotosha tafsiri ya matamshi ya mtalii
aliyekuwa amemaliza kutembelea Mamlaka ya Bonde la Ngorongoro (NCAA), ametiwa
mbaroni.
Video ya mwongoza watalii
huyo, ilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita, na kuzua
taharuki katika sekta ya Utalii nchini,huku wadau wengi wakitaka asakwe na
kukamatwa.
Katika
video hiyo, mtalii huyo ambaye jina lake halikupatikana mara moja, anaonekana
akisema safari yake nchini Tanzania imekuwa nzuri na watanzania aliokutana nao
walikuwa ni watu wenye upendo.
Akizungumza
na gazeti hili kwa simu leo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne
Maghembe, alisema mara baada ya kuona video hiyo kwenye mitandao aliagiza
akamatwe mara moja.
“Nilitoa
maagizo jana (juzi) usiku atafutwe na akamatwe na taarifa nilizopewa leo ni
kuwa ameshakamatwa kwenye gate (lango) la Nabi Serengeti na yuko rumande kule
Mugumu”alisema.